Mbunge wa Jimbo la Kawe (Chadema), Mhe Halima Mdee ameuponda uamuzi wa Serikali kutenga Sh495 bilioni katika bajeti ya Wizaya ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19 kununulia ndege mbili.
Mbunge huyo amesema Serikali inafanya hivyo wakati ikielewa wazi kuwa kununua ndege hizo kutalitia hasara Taifa.
Mhe Halima Mdee akizungumza katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo Leo Aprili 24, 2018, amesema hata taarifa za Msajili wa Hazina mwaka 2015/16, zinaeleza wazi kuwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) halina mpango wa biashara wala wataalamu.
Katika bajeti hiyo, ATCL imetengewa Sh495 bilioni kununua ndege mbili; moja aina ya Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na ndege kubwa ya masafa marefu aina ya Boeing 787-8 (Dreamliner), yenye uwezo wa kubeba abiria 262.
“Mnaeleza kuwa mmetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa ndege mbili. Mwaka jana bajeti ya 2017/18 kupitia wizara ya fedha mlitenga fedha zisizopungua Sh500 bilioni kwa ajili ya kununua ndege,” amesema Mhe Halima Mdee.
“Hoja si kupinga ununuzi wa ndege, hoja ni fedha hizi za ununuzi wa ndege zitazalisha au tunazipoteza. Taarifa ya ATCL inaeleza wazi kuwa haikuwa na mpango wa biashara. Yaani tunawekeza fedha katika shirika ambalo halina mpango wa biashara,”amesema Mhe Halima Mdee.
Mhe Halima Mdee ameongeza kuwa, “Shirika lina madeni lakini tunanunua ndege hizi. Bunge litekeleze wajibu wake. Hivi kilimo kinachoajiri Watanzania wengi tunakiwekea fedha kidogo lakini kwenye ndege ambazo tunajua tunakwenda kumwaga fedha chini tunawekeza Sh1 trilioni.”
Aidha Mhe Halima Mdee amesema iwapo fedha hizo zitagundulika kuwekezwa kinyume na taratibu hata kinga ya Rais haitasaidia kwa kuwa atashtakiwa.

No comments:
Post a Comment