Kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki, Lucas Mbedule amewaomba msamaha washarika wa Kanisa Kuu la Mtwara.
Februari 4, askofu huyo aliwaomba msamaha waumini ili wasiliumize kanisa hilo kutokana na mgogoro uliodumu kwa miaka miwili. Kabla ya kuingia kanisani, alilala kifudifudi katikati ya lango kuu na kusali.
Mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo aliwataka washarika hao kuwa na subira wakati akijiandaa kwenda kuzungumza nao.
Jana, Mbedule aliwaomba radhi waumini hao baada ya baraza la maaskofu kumtenga pamoja na wenzake wawili kwa tuhuma za usaliti unaohusishwa na masuala ya kisiasa kwa kutosoma waraka wa sikukuu ya Pasaka uliotolewa na baraza hilo Machi 24.
Mbali na Mbedule, maaskofu wengine ni Dkt Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), na Dkt Solomon Massangwa wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Katika mkutano wake uliofanyika Aprili 24 na 25 Jijini Arusha, baraza hilo la maaskofu wa KKKT liliwapa maaskofu hao muda wa hadi Septemba kuandika barua ya kueleza kama wanaukubali au kuukataa waraka ambao walishiriki kuuandaa wa ujumbe wa Pasaka na iwapo hawatafanya hivyo, hatua zaidi dhidi yao zitachukuliwa.
Katika ibada ya Jana, kwanza Mchungaji Yeriko Ngwema aliwasomea washarika salamu za pasaka zilizokuwa zitolewe na maaskofu wakati huo na kutaarifu kuwa ufafanuzi ungetolewa baadaye na Askofu Mbedule.
Mchungaji Ngwema aliwaambia washarika kama walivyosikia kupitia vyombo vya habari, maaskofu wa kanisa hilo walituma salamu za Pasaka kwa washirika, lakini kwa bahati mbaya na kwa sababu zilizojitokeza kwa wakati huo hazikusomwa kama baraza la maaskofu lilivyoagiza.
Alisema kwa njia ya barua aliyoisoma mbele ya washarika anawaomba radhi kwa kuwakosesha baraka za maaskofu.
“Pili, kwa njia ya barua hii mtambue ya kuwa mimi kwa neema ya Mungu nilitia saini kwa mkono wangu katika salamu hizo, hivyo niko pamoja na mkuu wa kanisa na maaskofu wote kuwasilisha salamu hizo kwenu,” alisema Ngwema wakati wa kusoma salamu hizo.
“Neema ya Mungu ikae kwa wingi juu yenu, Askofu Lucas Mbedule Yuda; Dayosisi ya Kusini Mashariki. Nakala kwa wakuu wa kanisa na kwa waheshimiwa maaskofu wote wa KKKT naziwasilisha salamu zetu, Amin.”
Alichosema Askofu Mbedule
Akizungumza na Mwandishi wetu baada ya ibada jana, Askofu Mbedule alisema sababu za kutosomwa salamu za Pasaka ni kutokana na hali ya kanisa ilivyokuwa kwa kipindi ambacho zilitakiwa kusomwa.
Alisema hajawahi kuwa kinyume cha maaskofu wenzake ndiyo sababu salama hizo zilisomwa jana baada ya hali ya kanisa kuonekana imeanza kuwa sawa.
“Sijawahi kuwa kinyume na maaskofu wenzangu, ndiyo maana hata hapa tumesoma, kilichofanya tusisome ni kwa sababu hali ya usalama ya dayosisi haikuwa sawasawa kulikuwa na migogoro ya ndani, mwingine anasema hatumtaki askofu sasa mnaposema tunasimama na kitu ni lazima tuwe tumeungana kama kanisa kwa pamoja.
“Aliyesababisha andiko lisisomwe si askofu, ni mkutano wa wachungaji wa dayosisi, tukasema kutokana na hali ya dayosisi haijawa stable (imarika) tunaona tuchelewe tusisome kwanza mpaka turudi kwenye amani ndipo tutasoma. Halikuwa ni agizo la askofu tuko pamoja tulichelewa ndiyo maana hata umeona amesoma askofu msaidizi,” alisema Askofu Mbedule.
“Kosa letu sisi ni kwamba tulipoamua tusisome wakati huu, hatukuomba tukaonekana kama tumefanya tatizo, tuliamua kutosoma kwa sababu zetu hatupingani na kanisani.”
Dayosisi ya Kaskazini Kati
Baadhi ya waumini wa Dayosisi ya Kaskazini Kati walieleza kushtushwa na taarifa ya kutengwa Askofu Massangwa.
Wakizungumza baada ya ibada katika Usharika wa Mjini Kati, Arusha walisema kutosomwa kwa waraka huo kulitokana na askofu kufiwa na kaka yake.
Jeremiah Kaaya, muumini wa ushirika huo alisema wakati wa pasaka, Dk Massangwa alifiwa na kaka yake na msiba huo ulihudhuriwa na maaskofu wengine hivyo anadhani hiyo ndiyo sababu.
Muumini mwingine wa kanisa hilo, Yohana Shirima alisema anaamini Askofu Massangwa hawezi kujitenga na uamuzi wa maaskofu wenzake na kilichotokea ni upungufu.
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mjini Kati, Lembrice Pallangyo alisema: “Mimi si msemaji wa dayosisi, lakini ni kweli kipindi cha Pasaka askofu alikuwa na msiba wa kaka yake na alikaa msibani kwa siku kadhaa eneo la Nduruma nje ya Jiji la Arusha.”
Dk Massangwa alichaguliwa kuwa askofu wa dayosisi hiyo mwaka juzi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk Thomas Laizer.

No comments:
Post a Comment