Licha ya jitihada za Benki Kuu kuboresha mazingira ya biashara, benki kubwa za biashara nchini bado hazijaanza kutengeneza faida kubwa kama zamani.
Kwa mujibu wa taarifa za hesabu za kampuni kwa robo ya kwanza ya mwaka huu zilizotolewa leo, Jumatatu Aprili 30, faida ya baadhi ya benki kubwa; CRDB na NMB imeshuka.
Wakati faida ya CRDB ikipungua kwa takriban nusu ile ya NMB imeshuka kwa robo katika miezi mitatu ya kwanza mwaka huu huku NBC ikitengeneza zaidi ya mara 10 ya faida iliyopata mwaka jana.
Taarifa zinaonyesha faida ya CRDB baada ya kodi imepungua kutoka Sh26.188 bilioni iliyopata mwaka jana mpaka Sh13.6 bilioni robo iliyoishia Machi wakati ile ya NMB ikipungua kutoka Sh40.9 bilioni mpaka Sh31.687 bilioni ndani ya kipindi hicho.
Hata hivyo, tofauti na benki hizo, katika kipindi hicho, faida ya Benki ya NBC imeongezeka kutoka Sh517 milioni ilizopata mwaka jana mpaka Sh5.8 bilioni robo iliyoishia Machi mwaka huu.
Benki hizo tatu kwa pamoja zina ukubwa wa asilimia 40 ya sekta nzima yenye zaidi ya taasisi 50 za fedha.
Kwa miaka miwili iliyopita, sekta ya fedha nchini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ongezeko la mikopo chechefu, kutoimarika kwa mikopo iliyoelekezwa sekta binafsi hivyo kupungua kwa faida huku baadhi zikipata hasara.
Uwiano wa mikopo isiyolipika na jumla ya mikopo yote ulifika wastani wa asilimia 9.5 Desemba 2016 ukiwa umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 6.4 mwaka 2015 kiasi ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na ukomo wa asilimia tano uliowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kutokana na mwenendo mbovu baadhi ya benki zilipungukiwa mtaji kiasi cha kushindwa kujiendesha na kuilazimu BoT kuzifungia benki
tano mwaka jana na kuziweka nyingine tatu chini ya uangalizi wake.

No comments:
Post a Comment