Walimu wapewa onyo kuhusiana na siasa. - KULUNZI FIKRA

Friday 2 March 2018

Walimu wapewa onyo kuhusiana na siasa.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Valerian Juwal amewaonya walimu wa shule za msingi na sekondari kutojihusisha na masuala ya vyama vya kisiasa mashuleni.

Valerian amesema kuwa walimu kujihusisha na masuala ya kisiasa wakiwa mashuleni kunapelekea walimu kushindwa kufikia malengo yao.

“Walimu acheni tabia ya kujiingiza kwenye vyama vya kisiasa na kuacha majukumu yenu ambayo yapo kwa mujibu wa sheria na taratibu za ajira kwa kuwa mnapopatwa na matatizo hakuna wa kuwatetea zaidi ya mwajiri,“amesema Juwal kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Walimu wilayani Siha uliofanyika Jumanne ya wiki hii.

Kwa upande mwingine, Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Siha, Rose Sandi amesema kwa walimu kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa kunaweza kupelekea kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2009, inamtaka mtumishi yeyote wa umma kuwa na nidhamu na kutojihusisha na masuala ya siasa, hivyo kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

No comments:

Post a Comment

Popular