Simba yaweka lehani mbio za Ubingwa. - KULUNZI FIKRA

Friday 2 March 2018

Simba yaweka lehani mbio za Ubingwa.

 
Simba imezidi kuipa unafuu Yanga katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 dhidi ya Stand United

Walikuwa ni Simba walioanza kuliona lango la Stand katika dakika ya 6 ya mchezo kupitia kwa Ludit Mavugo, na baadaye dakika ya 26  Asante kwasi akafunga bao la pili na kuufanya mchezo kuwa 2-0.

Mambo yalianza kwenda kinyume kwenye dakika ya 36 baada ya Tariq kuifungia Stand bao la kwanza na baadaye kwenye dakika ya 41, Lulambo akaisawazishia Simba kwa njia ya kona iliyoingia kimiani moja kwa moja na kufanya dakika 45 za kwanza ziende kwa sare ya 2-2.

Kipindi cha pili kilianza vema upande wa Simba ambapo katika dakika ya 61, Nicholous Gyan alicheka na nyavu za Stand kwa kufunga bao la pili, lakini tena kwenye dakika ya 67, Bigirimana aliiswazishia Stand

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Simba SC 3-3 Stand United.

Kwa matokeo haya sasa Simba imefikisha alama 46, tofauti kwa alama 6 na Yanga iliyo na pionti 40.

No comments:

Post a Comment

Popular