Mwenyekiti wa Bavicha amvaa Naibu Waziri. - KULUNZI FIKRA

Friday 2 March 2018

Mwenyekiti wa Bavicha amvaa Naibu Waziri.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Patrick Ole- Sosopi amesema Baraza la Sanaa la Taifa linapaswa kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kusimamia majukumu ya kazi zao ndiyo maana walishindwa kuzichukulia hatua nyimbo zinazodaiwa kutokuwa na maadili.

Akizungumza na vyombo vya habari, Ole- Sosopi amesema hayo leo ambapo amesema kwamba kama nyimbo zimeweza kusikilizwa kwa muda mrefu basi ni wazi maadili na jamii zilishapotoka kwa muda mrefu kutokana na uzembe wa viongozi waliopaswa kuchukua hatua za haraka pindi  nyimbo hizo zilipoka.

Sosopi ameongeza kuwa hakuna mtu anayependa kusikia au kuona nyimbo zenye maudhui mabaya lakini anashangaza na jinsi baraza hilo linavyofanya kazi kwa mashinikizo huku akiongeza kwmba adhabu zilizotolewa kwa wasanii hazistaili.

Pamoja na hayo Sosopi amemtaka Naibu Waziri, Juliana Shonza kutengua adhabu yake hiyo kwani sheria haimpi yeye mamlaka ya kutoa adhabu alizotoa na badala yake wajibu huo upo chini ya BASATA.

Hapo jana Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo alitangaza kumfungia Msanii Hip Hop bongo, Roma Mkatoliki kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri huyo w kurekebisha wimbo wao wa 'KIBAMIA' waliouimba yeye na Stamina (ROSTAM)

No comments:

Post a Comment

Popular