Nape Nnauye afunguka kuhusu sekta ya utalii Nchini. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 22 March 2018

Nape Nnauye afunguka kuhusu sekta ya utalii Nchini.

 
Mbunge Mhe  Nape Nnauye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii amefunguka na kutoa ushauri wake kuhusu sekta ya utalii na kusema kuwa wanapofaya mabadiliko yoyote lazima wawe makini wasisumbue sekta hiyo.

Mhe Nape Nnauye amesema hayo alipokuwa akiongea na watendaji wa sekta ya utalii na kusema kuwa maboresho ambayo wanataka kufanya ni mazuri na yenye nia ya kutaka kuleta mabadiliko lakini lazima waangalie namna nzuri ili kutoleta shida kwenye sekta hiyo ya utalii nchini.

"Hayo maboresho tunayofanya yana nia njema na ni mazuri sana lakini wakati tunayatekeleza tuangalie tusisumbue image ya Indusrty, wakati wa kufanya tuangalie sura ya tasnia yenyewe ya utalii isisumbuliwe kwa sababu mnaweza kuwa na nia njema lakini katika mchakato wa kufanya maboresho yenu mkajikuta mmefanya Industry yenyewe mkaiacha hoi", alisema Mhe Nape Nnauye.

"Naamini Waziri ni mjanja kwa sababu hawa wateja wetu ni wateja wa shughuli za muda mrefu wakati mwingine wakiona mna maboresho yanasumbua wakisema wanapumzika wanaweza kumpumzika jumla kwa wakati tunafanya mabadiliko", alisema Mhe Nape Nnauye.

"Maboresho hayo tukumbuke tuna wateja ambao ni deligents kwa sababu uamuzi wa mtu kuja kutalii ni mtu kutenga pesa na kuamua kuja kutembea na anaweza akaamua kwenda sehumu nyingine vilevile sababu humlazimishi aje kwako" alisema Mhe Nape Nnauye.

"Nadhani wakati wa kutenda haya mambo tusiwasumbue wateja wetu na tuwashilikishe bwana tunafanya hivi kwa faida yenu na matokeo yake yatakuwa haya kama ni kuzuia kwa muda fulani matokeo yake yatakuwa haya mimi nadhani tutafika salama" alisisitiza Mhe Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment

Popular