Jeshi la polisi limetoa amri ya kukamatwa kwa wabunge wawili wa Chadema. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 22 March 2018

Jeshi la polisi limetoa amri ya kukamatwa kwa wabunge wawili wa Chadema.

 
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam  limetoa amri ya kukamatwa popote walipo kwa wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mbunge Kawe, Mhe  Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe  Ester Matiku, kutokana na kutoripoti polisi wiki iliyopita.

Wakili wa Chadema, John Malya amesema hatua hiyo inatokana na wabunge hao kushindwa kuitikia wito uliowataka kuripoti polisi wiki iliyopita kwa sababu walikuwa wakihudhuria vikao vya kamati za bunge vinavyoendelea Mjini Dodoma.

Aidha Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe  John Heche na Mbunge wa Kibamba, Mhe  John Mnyika wamewekwa chini ya ulinzi kusubiri maelekezo ya kwa nini hawakuhudhuria wiki iliyopita.

“Wiki iliyopita Jumanne, wenzao waliripoti Mhe  Heche na Mhe  Mnyika hawakuripoti walikuwa bungeni, lakini Leo wameripoti na sasa amekuja hapa Mkuu wa Upelelezi akasema mkae hapa msubiri maelekezo", amesema Wakili Malya.

“Halima ameshindwa kuripoti, yuko nje kwa matibabu na sisi ndiyo tuko hapa tunasubiri hayo maelekezo", amesema Wakili Malya.

Katika mwendelezo wa kuitikia wito wa kuripoti kituoni hapo, Leo Mwenyekiti wa Chadema, Mhe Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Vincent Mashinji wameripoti.

Wengine waliofika kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Ndugu Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

No comments:

Post a Comment

Popular