Viongozi wa chadema wamewasili kituo kikuu cha polisi. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 22 March 2018

Viongozi wa chadema wamewasili kituo kikuu cha polisi.

 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mhe Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho,Dkt Vincent Mashinji wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kutakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya kusubiri kinachoendelea.

Wengine waliofika kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ndugu  Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe John Heche.

Wabunge ambao walitakiwa kufika lakini wameshindwa kutokana na sababu mbalimbali ni Mbunge wa Kawe, Mhe  Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe Esther Matiko.

Wabunge waliofika kituoni hapo waliripoti wakiwa wameongozana na Wakili wao, Frederick Kihwelo.

No comments:

Post a Comment

Popular