Makonda amekuja na mkakati wa kuwakomboa Vijana. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 18 March 2018

Makonda amekuja na mkakati wa kuwakomboa Vijana.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema anaratibu kuanzisha mashindano ya kukimbia kwa vikundi vya Jogging Club vilivyopo katika Jiji lake ili kunusuru vijana hao wasiweze kujiingiza katika vishawishi vya wizi kutokana na wengi kukosa kazi

Paul Makonda ameeleza hayo Leo (Machi 17, 2018) wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kusema amegundua kuwepo kwa vikundi vingi vya vinavyofanya mazoezi ya kukimbia katika nyakati za asubuhi lakini jambo la kushangaza vijana hao wengi hawana kazi za kufanya pindi wanapokuwa wamemaliza kufanya mazoezi hayo.

"Vijana wengi wa 'Jogging Club' hizo wanafanya mazoezi asubuhi halafu hawana kazi za kufanya wanarudi vijiweni, hiyo salama maana unaweza ukashangaa wakajikuta wameanza kuwa na 'speed' kubwa na matokeo yake wakapita na mikoba ya wakina mama kama hawana kazi za kufanya", alisema Makonda .

"Kwa hiyo sisi tunaratibu na kupitia hadhara hii niwaambie wananchi kwamba tunapanga mipango kwa kila mwisho wa mwezi kuwepo na mashindano 'Jogging Club", alisema Makonda.

Pamoja na hayo, Paul Makonda ameendelea kwa kusema "kila 'Jogging Club' itakayofanikiwa kuongoza itapewa zawadi ya Milioni 10 kama mtaji wa kuanza kufanya shughuli za kujiendesha kiuchumi katika makundi hayo na tunaanza na wilaya ya Temeke kwa kuwa ndio inayoongoza kwa 'Jogging Club' katika Mkoa wa Dar es Salaam. kwa hiyo tutaifanya mwezi ujao na 'Jogging Club' zote za mkoa tutakutana Temeke".

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema hicho kiasi cha pesa kitakachotolewa kwa washindi ni kama motisha ya sehemu za kuzitambua 'Jogging Club' pamoja na kuiongezea nguvu za mtaji.

No comments:

Post a Comment

Popular