Shambulio la Tundu Lissu lawafanya wabunge waililie serikali. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 10 February 2018

Shambulio la Tundu Lissu lawafanya wabunge waililie serikali.

 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu ameeleza masikitikao ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kufuatia kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu mwezi Septemba mwaka 2017 maeneo ya Bunge Dodoma na kuleta mshtuko mkubwa kwa wabunge na wananchi kiujumla

Kamati imependekeza kwa kuwa hakuna sheria wala kanuni inayoelekeza wabunge kupewa ulinzi katika makazi yao na hivyo kulifanya jukumu la ulinzi na usalama wa mbunge kuwa jukumu lake mwenyewe na kwa kuwa kazi ya mbunge katika kuisimamia serikali inagusa maslahi binafsi ya watu na makundi ambayo yanaweza kujenga chuki dhidi yao, hivyo sheria ya haki kinga na madaraka ya bunge irekebishwe ili kuweka sharti la wabunge kupewa ulinzi hususani katika makazi yao wanapokuwa katika majukumu ya kibunge mjini Dodoma na katika maeneo yao ya uwakilishi

Pia kuwekautaratibu wa kuweka namba maalumu za usajili wa magari ya wabunge kama MB Muheza, MB Viti Maalum Mbeya n.k

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hoja ya wabunge kupewa ulinzi ni hoja ya msingi na serikali haiwezi kulipinga , lakini kuna miundombinu inatakiwa iwe imefanyika katika nchi ili uweze kufanya ulinzi kwa mbunge mmoja mmoja

Ametolea mfano Dodoma ambapo tayari walishakubaliana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kwamba maeneo wanakokaa wabungewataimarisha doria pindi ambapo wabunge wapo Dodoma

Na maeneo ambayo wabunge wanakaa kwa pamoja watawekia utaratibu wa askari kuwa katika maeneo hayo lakini utaratibu wa kuwa na ulinzi wa mbunge, mathalani katika kila jimbo ni jambo ambalo linahitaji miundombinu kwanza kabla ya kuweka utaratibu huo kwa kuwa askari watakuwa katika hatari ya kushambuliwa na hata kunyang'anywa silaha

Mwigulu amesema nchi ambazo mbunge anapewa ulinzi, mbunge anakaa kwenye makazi maalumu kama mkuu wa Wilaya ambapo inawezekana kupeleka ulinzi kwa kuwa ni eneo la serikali

No comments:

Post a Comment

Popular