Serikali yatoa adhabu Kali kwa askari wa Jeshi la polisi nchini. - KULUNZI FIKRA

Friday, 9 February 2018

Serikali yatoa adhabu Kali kwa askari wa Jeshi la polisi nchini.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kupitia Jeshi la Polisi nchini limewachukulia hatua mbalimbali za kinidhamu takribani askari 105 ikiwa pamoja na kuwafukuza kazi

Hayo yamebainishwa na  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe  Hamad Masauni katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa viti maalumu (Chadema) Sofia Mwakagenda alilotaka kufahamu kuwa kuna sheria yeyote ya nchi inayomruhusu Askari Polisi kumkamata mtuhumiwa, kumpiga na kumtesa kabla ya kumfikisha katika kituo cha polisi.

"Kwa mujibu wa mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kifungu cha 11 kinaelekeza namna ya ukamataji, kwamba kifungu hicho hakimruhusu askari kumpiga na kumtesa raia wakati wowote anapokuwa kizuizini. Kanuni za utendaji wa Jeshi la Polisi (PGO) askari yoyote anapobainika kufanya vitendo vya kupiga au kutesa raia huchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani", amesema  Mhe Masauni.

Pamoja na hayo, Mhe Masauni ameendelea kwa kusema "katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2017 jumla ya askari polisi 105 waliotenda makosa mbalimbali wamechukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa pamoja na kufukuzwa kazi".

Kwa upande mwingine, Mhe Masauni amesema muda mwingine aina ya ukamataji muharifu huwa inategemeana na muonekano wake ukoje.

No comments:

Post a Comment

Popular