Mtulia atoa ahadi nzito kwa wanakinondoni. - KULUNZI FIKRA

Friday, 9 February 2018

Mtulia atoa ahadi nzito kwa wanakinondoni.

 
"Ninapozungumza shida na matatizo ya wana Kinondoni siigizi kwa sababu ni mwenzenu nayajua,Kiongozi mzuri ni yule anayezijua na kuguswa na shida za Watu wake, mimi ni mfano wa kiongozi huyo", alisema Mtulia.

"Nilivunja kibubu na kwenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa, nikashinda na bomoabomoa ikazuiwa. Hii ilisaidia kuzuia bomoabomoa si tu Kinondoni bali nchi nzima", alisema Mtulia.

"Mrudishe Mtulia akajenge barabara, nipeni kura nikasimamie ufanisi wake, Matatizo ya Mto wa Ng'ombe yanaenda kuwa historia kutokana na Mto kwenda kujengwa upya na hatutakuwa na shida ya mafuriko na maji kujaa majumbani tena. Pesa zipo tayari, nipeni kura nikasimamie"  alisema Mtulia.

"Kiongozi wa upinzani hawezi kuleta maendeleo kutokana na kutokuwa na mahusiano mema na Serikali,nikishinda nitahakikisha suala la Bodaboda kugeuzwa gari la mshahara. Nitasimamia na kuzuia manyanyaso yao", alisemaMtulia.

"Nikishinda naenda kusimamia Manispaa itoe mikopo nafuu kwa Vijana na akina Mama waweze kujiajili,nitaenda kuhakikisha vituo vya bodaboda vinatambuliwa kwa kupewa namba maalum ya utambulisho", alisema Mtulia.

"Nimeamua kubadilisha gari ili kuhakikisha nawafikisha salama na mapema kwenye maendeleo wana Kinondoni, nawaombeni sana Februari 17 mkanipigie kura nyingi za ndio ili niweze kushinda na kuwaletea maendeleo ya kweli, Chagua Mtulia, Chagua CCM, Chagua Maendeleo"  alisema Mtulia.

No comments:

Post a Comment

Popular