Raia wa kigeni ahukumiwa kifugo cha Maisha kwa kusafirisha dawa za Kulevya. - KULUNZI FIKRA

Thursday 15 February 2018

Raia wa kigeni ahukumiwa kifugo cha Maisha kwa kusafirisha dawa za Kulevya.

 
Mahakama Kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi ,imemhukumu kifungo cha maisha jela ,Christina Biskasevskaja (26) raia wa nchi ya Lithuania baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin na Hydrochloride kinyume cha sheria .

Hukumu hiyo imetolewa jana Mahakama kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi na Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ,Aishieri Sumari ambapo upande wa utetezi ulikuwa ukiwakilishwa na Mawakili Patrick Paul na Gwakisa Sambo huku upande wa jamhuri ukiwakilishwa na Jopo la Wanasheria wa serikali wakiongozwa na Tamari Mndeme .

Akisoma hukumu ,Jaji Sumari alieleza kuwa mahakama imejiridhisha kupitia ushahidi usio na shaka uliowasilishwa na mashahidi wapatao saba wa upande wa Jamhuri unlimtia hatiani mshtakiwa huyo ambao ulieleza kukutwa na Dawa hizo zikiwa na uzito wa gramu 3775.26 na thamani ya sh za kitanzania Mil 169,886,700.

Biskasevskaja ambaye pia anatajwa kuwa msanii wa Muziki alikamatwa Agosti ,28 mwaka 2012 majira ya saa 9:16 za mchana katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akijiandaa kuelekea katika mji wa Brussels Ubeligiji kupitia Addis Ababa Ethiopia. Na Dixon Busagaga,Moshi.

No comments:

Post a Comment

Popular