Mugabe alalamikia serikali ya Zimbabwe kwa kumnyanyasa Mke wake. - KULUNZI FIKRA

Sunday 25 February 2018

Mugabe alalamikia serikali ya Zimbabwe kwa kumnyanyasa Mke wake.

Rais wa Zimbabwe aliyeondolewa madarakani na Jeshi, Robert Mugabe, amelalamikia Serikali ya nchi hiyo kumnyanyasa mkewe, Grace

"Mke wangu mpenzi Grace, amekuwa analialia kila siku, hawa wakubwa wanamnyanyasa na kumnyanyapaa, wanamuona hafai sasa," alilalamika Mugabe Jumatano ya wiki hii wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. Ametimiza miaka 94.

Alisema amechoka kubembeleza mkewe kwa kilio kinachosababishwa na watu aliowaita "wenye roho mbaya."

Mugabe aliwaeleza ndugu na jamaa zake wa karibu waliohudhuria sherehe ndogo, isiyokuwa mbwembwe kama illivyozoeleka wakati akiwa madarakani.

Alisema mkewe anaonekana hafai wakati amechangia kwa kiasi kikubwa amani na maendeleo ya Zimbabwe na watu wake.

Katika siku za hivi karibuni, Grace amekuwa akionekana kituko kwa Wazimbabwe baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa alikuwa 'kinara' na mshauri mkuu wa Mugabe kung'ang'ania madarakani na kulazimisha amrithishe uongozi wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular