Godbless Lema amjia juu Mnyeti. - KULUNZI FIKRA

Sunday 25 February 2018

Godbless Lema amjia juu Mnyeti.

Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe Godbless Lema ameikosoa kauli ya Mkuu wa Mkoa Alexander Mnyeti kuhusu kuwataka wamiliki ya migodi ya Tanzanite kuwalipa mishahara wachimbaji na endapo watashindwa kutekeleza hilo basi wakusanye virago vyao.

Mhe Lema amesema kwamba kaiui hiyo ya Mkuu wa Mkoa huenda itaweza kuua biashara ya Tanzanine na badala yake ameshauri udfanyike utafiti wa kina iiwa ni pamoja na kuitaka wizara husika kutafuta njia sahihi yenye faida kwa pande zote mbili.

Mapema Leo Mkuu wa mkoa Alexander Mnyeti alipokuwa akizungumza na wamiliki wa migodi, mameneja na wachimbaji katika mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro amesema utekelezaji wa agizo lake unapaswa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hakuna mjadala katika utekelezaji kwa kuwa kwa muda mrefu wamiliki wa migodi wamekuwa wakijinufaisha wao na familia zao bila kujali haki za wachimbaji.

Aidha Alexander  Mnyeti amenukuliwa akisema "Kama wewe huwezi kulipa mishahara ya wafanyakazi wa migodini ufungashe virago urudi nyumbani, ukatafute kazi nyingine ya kufanya,"

Ameongeza "Sheria haina huruma, mama mjane au mwanamke ni kule nyumbani huku machimboni anakuwa mkurugenzi wa mgodi, sina huruma kwa hilo walipeni mishahara wafanyakazi wenu,".

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Missaile Mussa amesema wachimbaji wa madini wanapaswa kulipwa mishahara kwa mujibu wa sheria ya kazi namba sita ya mwaka 2004.

No comments:

Post a Comment

Popular