Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe Dkt Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Mhe Dkt Faustine Ndugulile.
Wabunge waliohudhuria ni Mhe Hussein Bashe wa Nzega Mjini,Mhe Azzan Zungu (Ilala), Mhe Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Mhe Halima Bulembo (Mbunge wa Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
Wengine ni Mhe Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Mhe Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Mhe Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Mhe Rita Kabati ( Mbunge wa Viti Maalumu).
Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.
Mhe Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
Mhe Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.
“Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema Mhe Mapunda.
Mbunge wa Ilala Mhe Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.
Mhe Dkt Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”

No comments:
Post a Comment