Mkoa wa Mara ni moja ya kati ya inayovuma kwa kuwa na ukatili mkubwa kijinsia na kwa kilimo cha bangi pia.
Majaliwa alitoa nasaha hizo juzi wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, hapa Tarime.
Waziri Mkuu alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kilimo cha bangi vinaitia doa wilaya hiyo, hivyo hawana budi kuepukana navyo.
“Serikali inakemea vitendo vya ukatili, achaneni navyo," alisema Waziri Mkuu. "Mtu unamchapa mtoto makofi hadi anazimia, kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na pia kinaitia doa wilaya yenu.”
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwa ngazi ya mikoa Machi 8 mwaka jana, Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa) Edda Sanga, alisema mkoa wa Mara ni kinara kwa unyanyasaji na ukatili wa wanawake nchini.
Alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mapambano dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa juzi alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga kuendelea na msako wa mashamba ya bangi na mirungi na kuchukua hatua kwa watakaobainika kuendesha kilimo hicho.
Majaliwa alisema ardhi ya wilaya hiyo ni nzuri na inahimili kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama mahindi, mihogo, ndizi, kahawa, pamba, hivyo ni marufuku kulima bangi.
Pia Waziri Mkuu aliagiza kuchukuliwa hatua kwa wakandarasi waliotekeleza ujenzi wa miradi ya maji mkoani Mara kwa sababu wameijenga chini ya kiwango.
Majaliwa alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kupitia mabango wakidai kutonufaika na miradi ya maji katika maeneo yao licha ya Serikali kutoa fedha.

No comments:
Post a Comment