Furaha ya wakazi wa maeneo ya Kigoto, Mhonze na Kayenze, zote za Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza waliyoipata Oktoba 30 mwaka jana baada ya Rais John Magufuli kusitisha ubomoaji nyumba zao imeanza kufifia.
Hii ni baada ya Serikali kutangaza uamuzi wa kubomolewa kwa nyumba 1,600 za kaya zinaodaiwa kuvamia eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza, huku kaya 664 zinazodaiwa kuvamia eneo la Jeshi la Polisi katika Mtaa wa Kigoto zikiagizwa kusitisha uendelezaji wa maeneo yao kusubiri uamuzi mwingine.
Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvu alipotembelea na kuzungumza na wananchi wanaodaiwa kuvamia eneo la Jeshi la Polisi.
“Kuna kaya 664 zinazodaiwa kuvamia eneo polisi; kaya 461 zinatakiwa kuondoka. Naagiza msitishe zoezi la kuyaendeleza maneo haya kusubiri maamuzi mengine,” alisema Mhe Lukuvi na kuongeza;
“Nyumba 1,600 zinazodaiwa kuingilia eneo la uwanja wa ndege zitabidi kubomolewa.”
Aliwaeleza wananchi hao kuwa ziara yake ni agizo la Rais Magufuli la kukagua maeneo yanayodaiwa kuvamiwa na wananchi na kumpa taarifa kwa ajili ya uamuzi unaotarajiwa kutolewa ndani ya mwaka huu. Oktoba 30 mwaka jana, Rais Magufuli alisitisha ubomoaji wa nyumba za wakazi zaidi ya 3,000 wa maeneo ya Kigoto, Mhonze na Kayenze Manispaa ya Ilemela hadi hapo Serikali itakapotoa uamuzi mwingine.
“Inawezekana walifanya makosa. Lakini naagiza zoezi la kubomoa nyumba za wananchi lisitishwe hadi pale Serikali itakapotangaza uamuzi mwingine,” aliagiza Rais Magufuli. Rais Magufuli alitoa agizo hilo alipohutubia wananchi wa eneo hilo muda mfupi baada ya kuzindua daraja la waenda kwa miguu eneo la Furahisha baada ya kusoma ujumbe uliokuwa umeandikwa kwenye mabango yaliyokuwa yameshikiliwa na wananchi.
Katika agizo hilo, Rais Magufuli alisema ametumia mamlaka yake ya kisheria chini ya Sheria ya Ardhi namba 4/1999, Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5/1999 na Sheria na Mipango Miji ya mwaka 2007 inayompa mamlaka ya uamuzi katika masuala yanayohusu ardhi.
Rais pia aliziagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi; Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mambo ya Ndani ya Nchi; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela kukutana, kujadili, kukagua na kutoa mapendekezo ya kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wananchi taasisi za Serikali.

No comments:
Post a Comment