Waziri Kigwangala awajia juu mawazri wakuu. - KULUNZI FIKRA

Friday, 26 January 2018

Waziri Kigwangala awajia juu mawazri wakuu.

Mawaziri wakuu wastaafu ambao wamepata kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ni Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Sinde Warioba, John Malecela, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda. Wengine ambao tayari wametangulia mbele za haki ni Mwalimu Julius Nyerere, Rashid Kawawa na Edward Sokoine.

Makampuni ya uwindaji Aidha katika mazungumzo yake, Kigwangala pia ametoa siku saba kwa wamiliki wa makampuni matano ya uwindaji kujisalimisha bila kutuma wawakilishi kutokana na kuendesha shughuli kinyume na utaratibu. Kampuni hizo zinatuhumiwa kwa makosa tofauti yakiwemo uwindaji haramu, ubadilishaji wa umiliki wa vitalu vya uwindaji pasipo kufuata sheria, ujangili, udanganyifu, rushwa, uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori na uhujumu uchumi.

Waziri Kigwangala alitaja makampuni hayo kuwa ni Berlette Safari Corporation Limited ambayo ina vitalu vya Ruvu Masai GCA, Selous GR LL1, Selous GR LL2, Selous GR MT2 ambapo wamiliki wake na washirika wake ni Erick Pasians na wenzake. Kampuni ya Game Frontiers of Tanzania Limited yenye vitalu vya Moyowosi/ Njigwe GR 2, Rungwwa River GCA, Mbarang’andu WMA na Ugala GR E ambapo wamiliki wake ni Sheni na wenzake.

Kampuni ya Mkwawa Hunting Safaris Limited yenye vitalu vya Selous M1, Selous GRK4, Selous GR R1 ambapo wamiliki wake ni Howel na wenzake. Kampuni ya Tanzania Game Trackers Safaris Limited yenye vitalu vya Maswa Kimali GR, Maswa Mbono, Ugalla GR N, Ugalla GR S ambapo baadhi ya wamiliki na washirika wake ni Fredikin Family na wenzake.

Pia kampuni ya Wengert Windrose Safaris Tanzania Limited yenye vitalu vya Lake Natron GCA-North, Makere FR Uvinza OA na Mayowasi GRS ambapo ambapo baadhi ya wamiliki na washirika wake ni Fredikin Family na wenzake. Aliongeza: “Awadh na wenzake wa kampuni ya Green Miles Limited, Kuzena Robert ambao ni washirika wa Muhsin Shen, Solomoni Makulu, Siasa Shaban, Hamisi Ligagabile na mtumishi wa wizara, Alex Aguma,” wote hawa wajisalimishe na watahojiwa na timu maalumu itakayokuwepo wizarani.

“Kuna watu wanaodhani kuwa hawagusiki na sasa mimi ninaanza kushughulika nao ili mwisho mwa siku vikosi vilivyoko chini vipate nguvu ya kwenda mbele kwa kasi zaidi,” alisema Alisema kuna mkakati mahususi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori muda si mrefu kutakuwa na sheria ya mabadiliko kuhusiana na wanyamapori ili kuweza kuboresha utendaji.

Alisema wamekamata watuhumiwa 74 na washirika wao 949 na baadhi yao wamechukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani na wanaendelea kufuatilia na wengine wametoroka. Pia alisema wanakusudia kufanya uhifadhi kwa kurusha ndege zisizo na rubani ili kuzuia ujangili na kufunga kamera maeneo yote ili kudhibiti majangiri kama Serengeti na Ngorongoro ili kudhibiti majangili kuingia kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.

Aipa polisi siku saba Katika mazungumzo hayo pia ametoa siku saba kwa Jeshi la polisi kuwakamata watu waliohusika na mauajiya Mkurugenzi wa Palm Foundation, Wayne Lotter raia wa Afrika Kusini yaliyotokea Agosti mwaka jana na endapo wakishindwa kufanya hivyo, atashitaki kwa Rais Magufuli.

“Mimi majina yao nawafahamu, watatu wanahusika na kuendesha biashara ya ujangili ni matajiri wakubwa, taarifa hizi polisi wanazo lakini hawajawakamata watu hao, imekuwa muda mrefu na sisi tumechoka kusubiri nawapa siku saba wawe wamekamata watu hao,” alisema.

Tuhuma Tanapa Waziri huyo pia alielezea tuhuma zilizotolewa na kituo cha utangazaji cha ITV News cha Uingereza, kuhusu baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TANAPA), kuhusika kwenye mtandao wa mauaji ya Tembo. Alisema baada ya kutolewa tuhuma hizo, serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imeunda timu ya uchunguzi ya watu sita, itakayoongozwa na aliyekuwa Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Waziri huyo alisema kamati hiyo itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu ya kutokea mauaji ya tembo karibu na vituo vya walinzi ambapo tume hiyo itafanyakazi ndani ya siku 14 kisha kuwasilisha ripoti kwangu,” alisema. Kuhusiana na Nyalandu Akizungumzia kuhusu suala la aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu alisema suala kuhusu waziri huyo wa zamani aliwahi kulizungumzia bungeni lakini anashangaa kwa nini hatua hazichukuliwi dhidi yake.

“Kama nimesema jambo bungeni maana yake limekuwa public maana yake taarifa zimewekwa wazi kwa hiyo wanaohusika wanapaswa kuchukua hatua, wakitaka niwape maelezo ya kina nipo wakitaka ushahidi upo”. “Mtu amekaa na ‘Document’ ya kusaini tozo mwaka mmoja na nusu amekaa nayo mezani halafu sisi tunakuona upo katika mahotel kwa hiyo Serikali imekosa mapato kwa zaidi ya Shilingi bilioni 30 kwa sababu tu mtu hakusaini.

No comments:

Post a Comment

Popular