Wazazi waandamana kwenda shule kuchukua michango yao. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 20 January 2018

Wazazi waandamana kwenda shule kuchukua michango yao.

 
Kutokana na kauli ya Mhe Rais Magufuli kuwa  shule zilizochangisha wanafunzi michango kuacha na kurudisha michango hhiyo Mara moja.

Jana siku ya ijumaa ilithibitika baadhi ya wazazi  katika halmashauri mji wa Mbinga waliandamana kudai fedha zao. Walimu wakuu waliokumbwa na dhahama ni shule za Nazareth, Kipika na shule nyinginezo za pembezoni.

Kwa upande wa shule ya msingi kipika wazazi walidai kufuata fedha ambazo walichangishwa sh. 20,000 kila mzazi.huku baadhi ya wazazi wakidai michango hyo walichangishwa kwa vitisho na wengine watoto wao wakirudishwa nyumbani kwa kukosa michango hiyo.

Busara za Mhe  Diwani wa Kata ya matarawe Leonard Mashunju zilifanikiwa kuwaondoa wazazi hao baada ya kuwaomba wazazi hao waende jumatatu kuchukua fedha zao.

Shule ya msingi Nazarethi ambayo ipo mita 400 toka ofisi za elimu na mita takribani 600 toka ofisi ya mkuu wa wilaya walifuata michango yao tsh. 21,000 ambazo walikuwa wanachangishwa ikiwa ni tsh. 10,000 kwa ajiri ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali, sh. 5000 kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa matundu ya vyoo na tsh. 6000 na mahindi kwa ajiri ya chakula.

Kwa upande wa shule nyingine wazazi walikutana na vitisho kwamba wazazi wanaoenda kudai fedha zao wanatishiwa watoto wao kufelishwa endapo wataonekana viunga vya shule. Hivyo watoto wao huwawahi wazazi wao mapema kabla hawajakaribia maeneo ya shule na kuwaomba warudi nyumbani.

Wazazi wengi walionekana kumshukuru na kumpongeza Mhe Rais Magufuli kwa kuwa na macho makubwa ya kuweza kuona kinachofanyika hadi chini. Wamempongeza kwa jinsi alivyoongea kwa hisia Kali suala hilo kwani amewathibitishia wanyonge kwamba ana uchungu wa dhati na wanyonge. Wengine walionekana wakienda mbali zaidi wakilaumu watendaji waliopewa dhamana kutotekeleza ipasavyo maagizo ya Mhe  Rais Magufuli anayo yatoa.

"Nchi ina wakuu wa wilaya, wakurugenzi, kamati za ulinzi na usalama ,maafisa elimu, waratibu walipaswa kusimamia maagizo ya Mhe Rais Magufuli  lakini hali imekuwa tofauti sana wananchi wanakandamizwa lakini hakuna anayejali,wote wapo likizo kuanzia waziri mwenye dhamana hadi wakuu wa wilaya", alisema mmoja wa wazazi hao.


No comments:

Post a Comment

Popular