Polepole atoa maagizo kwa viongozi wa CCM. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 20 January 2018

Polepole atoa maagizo kwa viongozi wa CCM.

 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wake wa NEC Itikadi na Uenezi, Ndugu  Humphrey Polepole kimewataka viongozi wake wa ngazi zote kuisimamia serikali katika ngazi zote na kuhakikisha wanajishughulisha na kutatua shida za wananchi kwenye maeneo yao.

Ndugu Polepole ameeleza hayo katika kikao kilichokuwa na lengo la kuimarisha na kukijenga chama hicho kilichofanyika Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Moshi mjini huku kikiongozwa na mwenyekiti wa wilaya Alhaji Shamba na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Peter Patrick Boisafi, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Kippi Warioba, wazee mashuhuri, viongozi wa dini pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata.

"Mwaka huu ni wa ujenzi wa chama, kukumbushana misingi ya CCM, kutazama madhaifu na umadhubuti wake katika maeneo yote. Wanachama na viongozi muelewe Katiba, kanuni, taratibu na miongozo ya chama na zaidi viongozi msikilize watu na mtatue shida zao.
Kiongozi wa CCM soma na somo kubwa kabisa lipo kwa watu, kuwasikiliza, kuelewa shida zao na malalamiko yao, hakuna somo zuri kama hilo kutoka kwa watu", alisema Ndugu  Humphrey Polepole.

Kwa upande mwingine, Polepole amewasisitiza wajumbe walioweza kuhudhuria kikao hicho dhana ya CCM ambayo ni kuisimamia serikali katika kila nyanja.

No comments:

Post a Comment

Popular