SERIKALI imetekeleza kwa vitendo ombi lililotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mhe Amina Mollel alipokuwa bungeni mwaka jana la kutaka kijengwe kituo cha afya Nduruma.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe Selemani Jafo juzi. Alisema mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itaona umuhimu wa kujenga kituo kikubwa cha afya eneo hilo la Nduruma ili kuwapunguzia adha wananchi waliokuwa wakifuata huduma za afya wilayani Arumeru ambapo ni mbali na eneo lao.
Pia Waziri huyo alisema wizara yake imetoa Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitakuwa na jengo la upasuaji, wadi ya watoto na chumba cha kuhifadhia maiti ili kuondoa kero ya ukosefu wa kituo cha uhakika kwa wananchi hao.
Akizungumza jana kwenye zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo hicho, Waziri alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijijini, Dkt Wilson Mahera kupeleka watalamu wa afya wanne Hospitali ya Rufaa KCMC ili wajifunze kozi ya muda mfupi ya kutoa huduma za usingizi kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji kwenye hicho.
Alisema: “Nataka waatalamu wa kituo cha afya Nduruma waende KCMC wakapate ujuzi wa kutoa huduma za usingizi kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji.” Awali Mkurugenzi wa Arusha, Dkt Kazeri alisema kituo kilizinduliwa mwaka 2014 na kuhudumia wakazi 14,000 na kuhudumia zahanati tano zilizopo katika maeneo mbalimbali huku kikiwa na watumishi 11 wa kada mbalimbali.

No comments:
Post a Comment