Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imezifunga na kuzifutia leseni za huduma za kibenki na kuwekwa chini ya mufilisi benki zifuatazo Convenant Bank for Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited na Meru Community Bank Limited.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BOT, hatua hii imetokana na benki hizo kufilisika na hivyo kwenda kinyume na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Kifedha ya mwaka 2006.
“Kwa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu Na 41(a) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa Mfilisi kuanzia tarehe 4 Januari, 2018.” imesema taarifa hiyo.
“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.” “ BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta utulivu katika sekta ya fedha” iliendelea kusema taarifa hiyo.

No comments:
Post a Comment