Mrema afika kituo cha polisi kufungua kesi ya kuzushiwa kifo. - KULUNZI FIKRA

Friday, 12 January 2018

Mrema afika kituo cha polisi kufungua kesi ya kuzushiwa kifo.

 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ,Augustine Mrema leo ameripoti rasmi tukio la kuzushiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii katika kituo cha polisi cha OysterBay kilichopo jijini Dar es salaam .

Mrema amesema taarifa hizo zilizushwa na kutengenezwa na baadhi ya wapinzani wanzake wasiomtakia mema Mhe Rais Magufuli kwa lengo la kuwafanya watanzania wasisikilize mazungumzo kati ya Mh Rais Magufuli na waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowasa badala yake wajadili kifo cha chake kitu ambacho si sahihi

No comments:

Post a Comment

Popular