Haukumiwa miaka 36 Jela kwa kosa la kumtorosha mwanafunzi. - KULUNZI FIKRA

Friday, 12 January 2018

Haukumiwa miaka 36 Jela kwa kosa la kumtorosha mwanafunzi.

 
Mahakama ya Wilaya ya Lindi imemhukumu mkazi wa kijiji cha Majengo Mkoani Mtwara Saidi Chindu (19) kifungo cha miaka 36 jela baada ya kupatika na hatia ya kubaka na kumtorosha mwanafunzi wa Sekondari (jina limehifadhiwa)

Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mkazi Erasto Phili baada ya kurudhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Kabla ya Phili hajatoa hukumu hiyo mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea na kujdai kuwa ametiwa hatiani kwa kuwa hajui kuzungumza

Baada ya utetezi huo hakimu Phili alimuuliza mwanasheria wa serikali Abruhamani Mohamed iwapo anakumbukumbu ya makosa ya zamani kwa mshitakiwa na kujibu hana na kuomba apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa wengine walio natabia kama hiyo pamoja na kuwalinda wanafunzi wakike waweze kuendelea na masomo

Akitoa hukumu wakili Phili alisema mahakama inamtia hatiani mshitakiwa kutumikia kifungo cha miaka 36 jela kutokana na kosa alilotenda

Alifafanua kwamba kosa la kwanza la kubaka mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 na kosa la pili la kumtorosha mwananfunzi adhabu yake ni miaka sita jela hivyo kufanya jumla ya miaka 36.

No comments:

Post a Comment

Popular