Mbunge wa Chadema ameapa mbele ya wananchi kutohamia CCM. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 14 January 2018

Mbunge wa Chadema ameapa mbele ya wananchi kutohamia CCM.

 
 Mbunge wa Jimbo la Mbozi kupitia CHADEMA, Mhe Paschal Haonga amesema hana mpango na wala hayuko tayari kuhama chama hicho na endapo ikatokea akahama chama hicho wananchi wachome moto nyumba yake anayoishi na familia yake.

Mhe Haonga ametoa kauli wakati akizungumza na wapiga kura wake katika mwendelezo wa mikutano yake jimboni humo.

Ametoa msimamo huo leo, Jumamosi katika harakati za kuwatoa hofu wapigakura wake baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mbunge huyo naye ni miongoni mwa wabunge wanaohisiwa kuendelea kukihama chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Popular