Mwenyekiti wa Chadema, Mhe Freeman Mbowe amesema siri ya mshikamano wa viongozi wa chama hicho ni kufanya kazi kama watu wa familia moja bila ya kujali nafasi zao za uongozi.
Mhe Mbowe amesema hayo Jana Jumamosi mara baada ya ibada ya mazishi ya mama mzazi wa wakili maarufu wa kujitegemea Peter Kibatala, Anastazia Mayunga iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Maria Consolata Parokia ya Sua.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Mbunge wa Morogoro Mjini(CCM), Mhe AbdulAziz Abood na wabunge wa Chadema, Mhe Joseph Mbilinyi, Mhe John Mnyika, Mhe Godbless Lema, Mhe Suzan Kiwanga na Mhe Devotha Minja.
Amesema Chadema imeguswa na msiba wa mama wa wakili huyo ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akikisaidia chama katika kutetea kesi mbalimbali zinazowakabili viongozi na wanachama wa Chadema na ndio maana waombolezaji wengi waliohudhuria msiba huo ni kutoka Chadema .
Mwenyekiti huyo amesema kwa kutambua umuhimu wa wakili Kibatala chama kimeamua kuhairisha kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho ambayo ilipaswa kuketi leo Jumamosi ili kutoa fursa kwa viongozi wake wakuu kuhudhuria mazishi ya mama mzazi wa wakili huyo aliyefariki baada ya kuangukiwa na ukuta

No comments:
Post a Comment