Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Salim Ahmed Salim Jana amewaaga Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye kikao kilicho kuwa kinaendelea Jana mjini Dodoma.
Mhe Dkt Salim ameaga baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho. Waziri Mkuu huyo wa zamani amempongeza Mwenyekiti wa CCM Rais John Pombe Magufuli kwa uongozi wake ambao umekiwezesha Chama kuimarika.
Katika hatua nyingine Mhe Dkt Salim amewashukuru wajumbe wote wa Kamati Kuu na viongozi wa Chama kwa ushirikiano ambao wamemwonesha muda wote wa ujumbe wake.
Aidha Mhe Dkt Salim ameahidi kuendelea kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.
Tarehe 17 Desemba 2017
Hotuba ya Mhe Dkt Salim Ahmed Salim kuaga Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu
ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, Tarehe 17 Disemba 2017, Dodoma, Tanzania.
• Mhe Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli.
• Mhe Makamu Mwenyekiti, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Ndugu Ali Mohamed Shein.
• Mhe Makamu wa Mwenyekiti Ndugu Philip Mangula.
• Mhe Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
• Waheshimiawa Viongozi wakuu.
• Waheshimiwa wajumbe wa Kamati Kuu.
Awali ya yote ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru ndugu mwenyekiti kwa kutupa nafasi hii adhimu ya kutoa shukran zetu na kuagana rasmi. Nimeanza harakati mbalimbali za siasa tangia nikiwa kijana mdogo katika umri wa miaka 17 nikiwa mwanafunzi wa sekondari. Nimekuwa mwanaharakati wa taasisi mbalimbali za vijana zilizoshiriki kwa namna moja au nyingine katika vuguvugu la ukombozi wa Zanzibar.
Nikiwa kijana mdogo nilipata kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama cha ZNP maarufu kama Youth Own Union, Makamu wa Rais mwanzilishi wa Umoja wa Wanafunzi wa Zanzibar na pia Katibu Mtendaji wa Umoja wa Vyama tisa vya upinzani Zanzibar maarufu kama kamati ya vyama tisa ambayo mwenyekiti wetu alikuwa Mzee Abeid Amani Karume.
Nilianza kupata imani ya viongozi wakuu wa vyama kuanzia chama cha Afro Shirazi Party (ASP) ambapo Rais wa Kwanza wa iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume aliniamini na kuniteua kuwa balozi wa Zanzibar nchini Misri nikiwa na umri wa miaka 22.
Na baadaye kabla sijawasilisha hati zangu za utambulisho kwa Rais Gamal Abdul Nasser, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akaniteuwa kuwa balozi wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, wakati huo ikijulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Niliendelea kupata imani hiyo baada vyama vya TANU na ASP kuungana na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo wenyeviti wake kuanzia Mwalimu Nyerere akifuatiwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na baadaye Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete waliendelea kuniamini katika dhamana mbalimbali.
Hapa ningependa kutoa shukran za pekee kwa wenyeviti wote wa kamati maalum ya halmashauri kuu ya Taifa ya Zanzibar hususan Rais Ali Mohamed Shein ambaye katika kipindi hiki ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo na kupitia kwake pamoja na wajumbe wote kwa ushirikiano mkubwa ambao nimeupata kwa kipindi chote nilichoitumikia.
Ni katika nyakati mbalimbali za uongozi wa viongozi wangu hao nimekuwa mjumbe wa vikao vikuu vya maamuzi vya chama chetu. Nimekuwa Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje ya Chama, Katibu wa Tume ya Ulinzi na Usalama na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama.
Ndani ya Serikali nimekuwa balozi nikiwakilisha nchi yangu katika nchi za Misri, India, China na baadaye nikawa mwakilishi wa kudumu wa nchi yetu katika Umoja wa Mataifa. Nafasi ambayo nilitumikia kwa miaka kumi. Pia nimetumikia kama Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri Mkuu pekee kutoka Zanzibar na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kimataifa nimetumikia vipindi vitatu vya jumla ya miaka kumi na mbili mfululizo kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) sasa Umoja wa Afrika (AU). Nafasi ambayo niliweza kuipata kwanza kutokana na imani ya viongozi wangu kwangu na pia imani ya mataifa mengine ya Afrika kwa nchi yetu.
Hata katika kamati kuu hii inayomaliza muda wake sasa nilipata uteuzi na hatimaye kuchaguliwa kwa kura nyingi wakati nikiwa nje ya nchi kwa shughuli za kimataifa. Hii ni ishara kubwa ya imani ya viongozi wenzangu na wanachama wa chama changu kwangu ambayo daima nitaienzi.
Vilevile nimepata imani na ushirikiano mkubwa katika kipindi hiki cha uongozi wa Mwenyekiti wetu wa sasa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli ambaye ningependa kusema yafuatayo.
Kwanza, umekuwa kielelezo wa kivitendo katika kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye daima aliamini kuwa Chama Cha Mapinduzi kinapaswa kuwa sauti ya kuyasemea na kusikiliza madhila na matamanio ya wanyonge.
Uongozi wako ndani ya serikali umefanikiwa kurejesha nidhamu ya uchapakazi na utendaji wa kiutumishi ambao umeweza kuimarisha imani ya wananchi na hasa wananchi wanyonge kwa chama chetu. Juhudi zako za kurejesha nidhamu, maadili na uzalendo katika serikali, chama chetu na
miongoni mwa wananchi wetu zinapaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu.
Mageuzi unayoyaongoza ndani ya chama chetu yanatambua na kuendana na kilio cha muda mrefu cha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla ambao wamekuwa wakitamani kuona chama kinarejea katika misingi yake. Zaidi pia mageuzi hayo yanatambua umuhimu wa kutoa nafasi kwa vijana wetu. Ni
muhimu vijana watambue kuwa wanaaminiwa kama baadhi yetu tulivyoaminiwa.
Lakini ili kufanikisha hilo vijana nao wawe mstari wa mbele kupambana na yote ambayo yanakwenda kinyume na misingi ya chama chetu na maslahi ya nchi yetu. Juhudi hizi zinapaswa kuhakikisha zinasaidia katika kutatua changamoto zinazowakabili vijana wetu hususan suala la ajira.
Ni muhimu pia katika muktadha wa mageuzi yanayoendelea katika nchi na chama chetu kuhakikisha yanalenga kuimarisha umoja wa watanzania. Kwa hali yoyote vile tusikubali kugawanywa kwa kisingizio chochote kama vile ukabila, udini, ukanda na vingine vyote ambavyo vinaweza kutugawa. Ni muhimu kutokubali mgawanyiko wowote ule unaotaka kuleta mfarakano baina ya unguja na pemba au baina ya Tanzania bara na Zanzibar.
Tukumbuke kwamba chama chetu na serikali zetu tunakabiliwa na changamoto nyingi za nje na ndani tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Ni muhimu kwa chama chetu kujipanga ipasavyo ili tuweze kukidhi mahitaji ya watu wetu na kukabiliana kikamilifu na changamoto mpya za kisiasa, kijamii na kiuchumi katika muktadha wa dunia ya sasa ya mapinduzi ya kiteknolojia. Kwa maana hiyo tunahitaji uongozi madhubuti na makini. Kama alivyosema Mwalimu kuwa bila ya CCM imara tutakuwa na serikali legelege na hivyo kuhatarisha mustakabali wa nchi yetu.
Vilevile, katika kumuenzi Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere, ningependa kusisitiza utaratibu wako wa kuzingatia muda. Kwa kweli jambo hilo limetugusa sana hasa sisi tuliobahatika kuhudumia nchi yetu chini ya Baba wa Taifa ambaye daima alisisitiza sana umuhimu kuzingatia muda. Jambo hili ni muhimu kusisitizwa wakati wote ili kuhakikisha kuwa linakuwa sehemu ya maadili ya uongozi wetu na sehemu ya utamaduni wa wananchi wetu.
Kibinafsi nakushukuru kwa upendo na imani uliyonionyesha hasa nilipokuwa ninakabiliwa na changamoto za afya yangu. Kwa niaba ya familia yangu nakushukuru sana.
Kwa kumalizia ninaomba kusisitiza kuwa, yote haya niliyoyaeleza hapa yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi, wanachama na wananchi kwa ujumla katika wakati wote nikitumikia taifa langu na chama chetu. Nina ahidi kwamba uzalendo wangu kwa nchi yangu na imani yangu kwa chama changu vitadumu daima katika maisha yangu.
Ninapumzika hivi sasa lakini daima nitakuwa pamoja na wanachama na viongozi wenzangu katika kuhakikisha CCM inazidi kuimarika kwa maslahi mapana ya umoja, amani na maendeleo ya nchi yetu.
Kwavile sasa tuko katika kipindi cha mwisho wa mwaka nawatakia kila la kheri katika sherehe za Krismas na Mwaka Mpya.
Mungu Ibariki Afrika.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

No comments:
Post a Comment