UVCCM wafunguka mazito kwa Alberto Msando, wamtaka awaombe Radhi. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 16 December 2017

UVCCM wafunguka mazito kwa Alberto Msando, wamtaka awaombe Radhi.

 
 WARAKA WA WAZI KWA MHAMIAJI NDANI YA CCM BWANA ALBERT MSANDO

Salaam Kwako Wakili Msomi Ndugu Albert  MSANDO awali ya yote Nichukue nafasi hii Kukukaribisha katika Misingi, Falsafa, Dhana, Itikadi na Sera za Chama Cha Mapinduzi "CCM" Nasita kukukaribisha ndani ya Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi "UVCCM" nikijua wazi Umri wako Umevuka Rika la kikanuni kuwa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM.

Najua bado una Ugeni wa mambo katika Taratibu za Kimfumo na Kimuundo Juu ya Namna Tunavyoendesha Mambo Yetu Ndani ya CCM nimekuwa nikitizama mara kwa mara katika magroup ya whatsap ukijaribu kujenga hoja kuhusu vijana wa CCM na Dhana ya RUSHWA Unayosema Imetamalaki Ndani ya UVCCM.

Juzi nimeona Pale Ukumbini wakati wa mkutano Mkuu UVCCM TAIFA Ulipokaribishwa Usalimie ukanza kuhutubia badala ya kusalimia! Kwa Vijana wa CCM hatukushangaa sababu Tuligundua ni Changamoto inayokukubali katika Itifaki

Ndug yangu Msando kwanza nianze kwa Kukutaadhalisha Ufahamu Jambo la Kuambiana Ukweli Ni Jambo La Kimuongozo ambalo lipo ndani ya Dhana ya Katiba kama Mottor yetu "Nitasema Ukweli Daima Fitina Kwangu Mwiko" Usichulie Ushauri na waraka wangu huu kama jambo Ambalo ni binafsi, Nausema Ukweli Huu Katika Dhana Ileile na Kukosoa na Kukosilewa kama Muongozo wa Mwaka1994 unavyotutaka.

Najua Wewe ni Moja ya Watu Makini na Mweledi haswa,ukizingatia ni mwamasheria Nguli kwenye Sheria Haswa Legal Method Kuna Kitu Kinaitwa Legal Research Yani Tafiti ya Kisheria na Hata Huku kusiko kwa wanasheria Kuna Kitu Kinaitwa TAFITI siku zote ni kanuni inajieleza kwamba Matokeo ya Utafiti wowote hupingwa Kwa Tafiti Nyingine ya Kisayansi iliotoa Majibu Tofauti na Yale Ni Kanuni Hii ya "NO RESEARCH NO DATA NO RIGHT TO SPEAK"* Inayotuelekeza Kama Hakuna Research Hakuna Data na kama hakuna data hakuna haki ya Kuzungumza

Ndug Albert Msando Ni Vizuri Ukajipa Muda wa kujifunza kwa kufanya Tafiti Namna Taratibu za Chama na Jumuiya Katika Uandaajeli wa TAARIFA zake.

HOJA YA KWANZA KUHUSU UVCCM KUMPOTOSHA MHE RAIS

Taarifa inapofika kwenye mkutano mkuu wa UVCCM inapitia hatua zifuatazo
Sekretarieti UVCCM.
Kamati ya Utekelezaji.
sekretariet CCM.

Baada ya hapo inaenda kwenye mkutano miongoni kwa wajumbe wa kamati tekelezaji ya UVCCM ni SG wa CCM je wote hawa wamempotosha Rais?

Wakati unajenga Hoja yako ulisema "Vijana mnamdanganya Rais asitoke hapa ajue anavijana 6m wakati jeduali linasema 1.4m hai "

Elimu ndogo ujifunze taarifa za CCM zinaonyesha aina zifuatazo za wana Chama
Wananchama wote wenye Kadi.
Wananchama HAI.
wanachama walofariki.
Wanachama waloondolewa.

Ndugu Msando ni sahihi kabisa tukisema UVCCM inavijana 6m lakini walio hai ni 1.4m hawa ni wale ambao wamelipa Ada zao mpaka kufikia mwezi Dec ktk matawi Yao.

Kwahiyo vijana wa CCM hawajampotosha Ndg Rais Bali wewe ndo umempotosha Ndg Rais kwa kutafuta Kiki jifunze kuheshimu watu na utuombe Radhi

Ndugu Albert Msando Hoja Yako ya Pili ni Vijana wa UVCCM kushibdwa Kupambana na RUSHWA NA UFISADI nilikuwa najiuliza huyu jamaa anazipata wapi hizi taarifa zake.

Vijana hawa unaowatuhumu kwa Dhihaka mbele ya RAIS kwa madai ya kusema Uongo kwenye Taarifa yao na Kushindwa Kupigana na Rushwa
ndio Waliokipigania Chama Cha Mapinduzi Kwa Jasho na Damu Usiku ma Mchana Wakati Huo wewe ulikuwa Bize Kukwamisha Juhudi za Kimaendeleo Kupitia Upinzani.

Ibara ya Nane ya Kanuni ya Umoja wa Vijana Inasema Kazi ya Vijana Ni Kupekea Maelekezo kutoka Chamani na Kuyatekeleza.

Wakati Vijana wa CCM wakipokea Maelekezo ya Kukilinda na Kukisemea Chama Katika Mchakato wa Kutafuta Katiba Mpya na Kusimamia Agenda ya serekali Moja wewe na Mwenyeki wako ndani ya CCM pamoja na wapinzani Wengine Msimamo wenu Ulikuwa ni Kukwamisha Juhudi za Chama Cha Mapinduzi Kuleta Maendeleo na Kusimamia Agenda mama Zenye maslai Kwa Chama na Taifa.

Albert Msando Jifunze Kuheshimu Vijana wa CCM Brother Unapokuja CCM learn How To Respect Others

Taasisi ya CCM unayoiona Leo ni Nzuri na Imetengemaa ni Vijana hawa hawa unaowaona Mizigo ndio Walioijenga Miaka yote wewe na Mwenyeji wako Aliyekupandisha Jukwaani Mkiwa wapinzani wakubwa wa CCM na SEREKALI yake Jifunzeni kuwa na HESHIMA kwa Vijana wa CCM.

Msando wewe unayewanyooshea Vijana wa CCM mikono Kuhusu RUSHWA ulikuwa na Mgombea wako Juzi Katika harakati wa uchaguzi wa UVCCM mlikuja nae gari moja wewe na Genge lako Kuja DODOMA mgombea Huyu Naye alituhumiwa Kwa Rushwaa Sijui Kama ulishajisafisha na Dhambi hii?

Ni hawa Vijana waliozunguka Nchi Nzima Kuinadi Sera,Ilani na Kuuza Itikadi ya Chama na Kuanzisha MAGUFULI CLUB, SAMIA CLUB walijitolea bure kabisa wakati wewe ukihamahama Mara CHADEMA Mara ACT hawa walikuwa na Jukumu la Kujenga chama na serekali ya Chama Tawala.

Jifunze kutuheshimu Vijan wa CCM wakati Wewe umebebwa Kutoka DSM kwa gari nzuri uliyolipiwa na Ruzuku ya Chama Cha Mapinduzi, Ukagharamiwa Chakula Kizuri, Hoteli nzuri ya Kulala na Posho Ukiwa dodoma kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uvccm, Vijana hawa walishajitolea Bure kabisa kwa Hiyari na Mapenzi yao Kuzunguka Nchi Nzima kwa mapikipiki Kukisemea Chama Kueneza Sera na msimamo wa Chama.

Ndugu Albert Msando Heshimu Vijana wa CCM ili nao wakuheshimu
Historia yako ukiwa CHADEMA na Ukiwa ACT Ni Chafu na Inajulikana ! Swala la Maadili na Uadilifu sio Kuhusu Uongo na Rushwaa pekee bali Hata "UFUSKA,UHUNI UZINIFU,UASHERATI (Ngono ,Pombe)" Vyote hivi vikizidi ni Utovu wa Nidhamu.

Hii Moral Authority ya Kusimama na kuwashutumu Vijana unatoa wapi! Sio Wewe Ndug Albert Msando Uliye jiuzuri kwa skondo ya Ulevi,usherati na Ufuska kwa kujirekodi na mwanamke Anayejinasibisha kufanya biashara ya mwili wake!

Please Jiheshimu na Kwa Heshima uliyonayo kwa jamii japo ni Kidogo basi fanya hima Utuombe Radhi Msando kwanza kwa Kumpotosha RAIS na Pili kuwatuhumu vijana waCcm Kukumbatia Rushwa.

hawa vijana waliomba Uanchama katika Mchakato wa kikatiba ngazi ya Tawi wakajadiliwa wakaonekana wanasifa kisha wakapewa Uanachama hawa Vijana hawakushawishiwa kujiunga CCM kwa fedha,mali au ahadi ya Vyeo wengi wao wamejitolea Muda, nguvu, mali na Maarifa yao Kukijenga Chama hiki tangu Utoto wao bila ujira kama ilivyo kwenu Ingependeza zaidi Ukiwaheshimu UVCCM.

Ndugu
Bombokojr Kamarade
13/12/2017
Muheza Tanga

No comments:

Post a Comment

Popular