Mbunge wa zamani wa Kigoma (NCCR-Mageuzi) amekanusha kuhamia CCM. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 17 December 2017

Mbunge wa zamani wa Kigoma (NCCR-Mageuzi) amekanusha kuhamia CCM.

 Mbunge wa zamani wa Muhambwe mkoani Kigoma (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa yeye amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM.

Akizungumza na kulunzifikra blog Jana Jumamosi Desemba 16, 2017 amesema ana imani na upinzani imara. Ametaka kupuuzwa kwa taarifa hizo kuwa anakwenda CCM kuunga mkono jitihada za Mhe Rais Magufuli.

"Msimamo wangu upo palepale na kama wamezusha ni wao na sababu zao. Watu wengi sana wamenipigia simu kuniulizia kuhusu jambo ili. Sijaeleza lolote kuhusu mimi kuhama NCCR-Mageuzi. Watanzania tunahitaji upinzani imara kuhama hatumsaidii Rais Magufuli, unaweza kumsaidia na kumuunga yale anayofanya ukiwa hukuhuku upinzani", amesema Mkosamali.

No comments:

Post a Comment

Popular