Rais Magufuli: Kamwe siwezi kuifuta jumuiya ya Wazazi. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 12 December 2017

Rais Magufuli: Kamwe siwezi kuifuta jumuiya ya Wazazi.

 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli amesema hawezi kuifuta Jumuiya ya wazazi ya Chama hicho katika kipindi chake cha kuwa Mwenyekiti.

Mhe Rais Magufuli ameyasema hayo Jana mjini Dodoma wakati anafungua mkutano wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM ambao ni mwendelezo wa mikutano ya uchaguzi wa Jumuiya mbalimbali za Chama hicho.

“Jumuiya hii ilianza mwaka 1955 ikiwa inaitwa Tanganyika African Parent Associations (TAPA), na aliyeianzisha ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na alifahamu kwanini ilianza nikiifuta nitakuwa nimekosa busara na nitalaaniwa”, amesema Mhe  Rais Magufuli.

Aidha Mhe Rais Magufuli ameongeza kuwa “Napenda niwahakikishie Jumuiya hii itaendelea kusimama kama zilivyo Jumuiya nyingine ndani ya Chama”, ameongeza Mhe Rais Magufuli.

Aidha Mhe Rais Magufuli amesifu mafanikio mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa na Jumuiya hiyo ikiwemo kumiliki shule mbalimbali pamoja na Chuo cha Sanaa cha Kaole kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Popular