Bashe: Sisi tulishindwa. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 12 December 2017

Bashe: Sisi tulishindwa.

 
 Mbunge wa Nzega mjini Mhe Hussein Bashe amefunguka na kumpa wosia Mwenyekiti mpya wa  (UVCCM) Kheri James kuwa amepata nafasi hiyo hivyo aitumie vizuri kuhakikisha UVCCM wanakuwa waasi wa udhalimu wa serikali na viongozi mbalimbali.

Mhe Bashe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa wao walijaribu kufanya hivyo lakini walishindwa ila anaamini kutokana na uwezo wa Mwenyekiti mpya wa UVCCM anaweza kutimiza hilo na kuhakikisha haki inasimamiwa vizuri.

"Mdogo wangu umechaguliwa na vijana ukiwa huna kitu zaidi ya historia yako nafasi ulizopitia zimekupa fursa ya kujua maisha Mama. Mabula alikupa fursa ya kukutana na machinga, bodaboda, wasomi na wasiokuwa wasomi nenda kaifanye UVCCM daraja la wote wasomi na wasiokua wasomi. Nenda kasimamie haki nenda kaifanye UVCCM 'a real speaker of Justice a real watchdog wa Chama, mlinzi wa Chama na Serekali UVCCM should be a rebels against all Injustice hata Kama tunafanya sisi wabunge ama Chama ama Serikali go stand for wat is right na hiyo ndio historia ya UVCCM sisi kaka zako tulishindwa ndani ya mioyo yetu tunajua tulishindwa kufanya vizuri bali tutakupa support kwenye kutimiza wajibu Wako" aliandika Mhe Bashe.

Mbali na hilo Mhe Bashe ameendelea kumsisitiza Mwenyekiti mpya wa UVCCM kuwa imani aliyopewa na vijana ahakikishe anaitumia vizuri na asimuangushe Mhe Rais John Pombe Magufuli ambaye aliwataka vijana kufanya mabadiliko ya viongozi ambao wataleta mabadiliko ndani ya chama na Umoja huo wa vijana.

No comments:

Post a Comment

Popular