Mkuu wa mkoa wa Simiyu akanusha kukamatwa na Takukuru. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 December 2017

Mkuu wa mkoa wa Simiyu akanusha kukamatwa na Takukuru.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amekanusha taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa amekamatwa na Takukuru.

Taarifa hizo zinaelezea kuwa Mtaka amekamatwa na Takukuru kwa kugawa fedha kwenye uchaguzi wa UVCCM.

Kutokana na taarifa hizo Mtaka amesema,"kuna taarifa zinasambazwa kwamba nimekamatwa na Takukuru nikigawa fedha kwenye uchaguzi wa UVCCM ni uzushi na uongo wa kupuuzwa".

No comments:

Post a Comment

Popular