Bavicha wafanya mabadiliko makubwa. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 2 December 2017

Bavicha wafanya mabadiliko makubwa.

Kamati utendaji ya baraza la vijana wa chadema (Bavicha) limemchagua, Patrick Ole Sosopi kuwa mwenyekiti wa baraza hilo kuchukua nafasi ya Patrobasi Katambi aliyehamia chama cha mapinduzi (CCM).

Kamati hiyo pia leo Desemba 2 2017, imetangaza kuziba nafasi ya makamu mwenyekiti kwa kumteua John Pambalu, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Ole Sosopiambaye amekuwa mwenyekiti wa baraza la vijana wa chadema (Bavicha). Viongozi hao wameteuliwa kuongoza baraza hilo kwa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa Bavicha, Julius Mwita amesema uamuzi huo uliofanyika jana kufuatia kikao cha dharura cha kamati hiyo ya utendaji.

Amesema baraza hilo mojawapo ya taasisi imara na itaendeleza mapambano."Tunawahimiza vijana wa chadema na vijana wote wa Tanzania wasimame kidete kwenye kazi ya kuijenga na kuipigania demokrasia ya nchi yetu katika misingi ya utawala bora na haki za binadamu".

Kwa upande wake Ole Sosopi amesema katika uongozi wake atahakikisha baraza hilo linarudi kwenye misingi imara na kuongoza mapambano ya kudai demokrasia.

Amesema akiwa mwenyekiti hata vumilia kuendelea kuona uonevu wanaofanyiwa wanachama wa chadema.

"Bavicha inaenda kuwa taasisi imara na bora zaidi baada ya kuondoka Katambi. Tunakwenda kupambania demokrasia ya nchi hii, tutawashawishi vijana kuwa wamoja kulitetea Taifa bila kujali maslahi ya vyama vyetu", amesema Ole Sosopi.

No comments:

Post a Comment

Popular