Mbunge wa Chadema amtaja mtu aliyetaka kumuua Tundu Lissu. - KULUNZI FIKRA

Friday, 15 December 2017

Mbunge wa Chadema amtaja mtu aliyetaka kumuua Tundu Lissu.

 
 Mbunge wa Serengeti, Mhe Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) amefunguka na kutaja sifa za mtu ambaye alitaka kumuua Tundu Lissu na kusema mtu huyo alishindwa kutekeleza hilo kwa kuwa Mungu hakupanga Lissu aondoke kwa kipindi hicho.

Mhe Marwa Ryoba amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa hospitali ya Nairobi Kenya na kusema kuwa Mbunge huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kutolewa risasi 16 mwilini.

"Mzee wa chuki na visasi walitaka akumalize lakini Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo akasema HAPANA, kazi niliyokutuma hapa duniani haijakamilika, nenda kaikamilishe kwanza ndo uje kwangu. Kamanda Tundu Antipas Mughwai Lissu anaendelea vizuri. Pamoja na risasi kumi na sita zilizotolewa mwilini bado hakufa haya ni maajabu ya Mungu tu. Bwana Yesu asante kwa uwezo wako unaozidi fahamu za madictotar.
Dictator uchwara don't play with God who is the owner of everything including you", aliandika Mhe Marwa.

Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, baadaye alisafirishwa na kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi ambapo mpaka sasa anapatiwa matibabu huko.

No comments:

Post a Comment

Popular