Live: Yaliyojiri kwenye mkutano wa Mbunge wa Chadema na waandishi wa habari. - KULUNZI FIKRA

Friday, 15 December 2017

Live: Yaliyojiri kwenye mkutano wa Mbunge wa Chadema na waandishi wa habari.

 Upendo Peneza: Anasema tunaenda kupoteza pesa za marudio ya uchaguzi kwa wabunge waliojiuzulu kwani gharama za uchaguzi ni za wananchi.

 Anasema yeye haondoki Chadema, habari zilizotolewLive a ni kuwa anaenda CCM ni uzushi.

Amesema anachukizwa na tabia ya wabunge wanaohama kwa sababu wanawaumiza wananchi kwa kutumia gharama kubwa katika uchaguzi. Fedha hizi zingeenda kujenga shule na hospitali. "Tumeendelea kuona wabunge wakihama vyama. Taifa linaingizwa kwenye pressure ya uchaguzi hata kabla ya muda. Tulidhani ingekuwa ni mda wa sisi wabunge kufanya kazi za maendeleo lakini tumekuwa tukipoteza mda wa kuhama vyama"

 Anasema wanaondoka upinzani wamehongwa na kununuliwa na CCM. Anasema kulikuwa na rumors za yeye kwenda CCM sasa amekuja kukanusha.

 Anasema wabunge hao waliohama wangempongeza Rais Magufuli wakiwa katika vyama vyao.

Anaangalia namna ya kupitia Katiba kama wanaweza kuzuia uchaguzi wa marudio kwa wabunge waliohahama. Anaongea na wanasheria kumsaidia kufikia azma yake ya kuzuia Marudio ya Uchaguzi kwa Waliojiuzulu.

Anasema alichokisema ni msimamo binafsi sio wa chama chake.

Nimehusishwa kuhama Chadema,Mimi sihami chadema kwa sababu nina amini katika Chadema.Nimekuja kuwaambia watanzania kuhusu utapeli wa hawa wanaohamahama vyama kwa sababu tu ya kumuunga mkono Rais.

CCM iache kurubuni na kuhonga watu ili kuwanunua wahamie chama Cha mapinduzi.

 Nakubaliana kuwa Kwenye vyama vya siasa kuna changamoto, Hata ndani ya Chadema kuna changamoto lakini nitavumilia sitahama chama.

No comments:

Post a Comment

Popular