LHRC: Uchaguzi mdogo wa madiwani umetoa picha kamili ya uchaguzi ujao. - KULUNZI FIKRA

Friday, 1 December 2017

LHRC: Uchaguzi mdogo wa madiwani umetoa picha kamili ya uchaguzi ujao.

 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika uchaguzi mdogo wa madiwani.
Ukiukwaji huo ni kama watu kupigwa na kutekwa na vyombo vya dola na wafuasi wa vyama vya siasa.

Wametoa mfano kata ya Kitui Iringa vijana wa CCM waliwavamia na kuwateka wanachama wa CHADEMA waliofahamika kwa majina ya Eliza Nyenza na Martha Francis na kuwapora na kuwanyanganya simu zao na kuwatupa katika msitu wa Kilolo.

Kushambuliwa kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Daudi Igogo na jeshi kumkamata na kumshikilia Alex Kimbe.

Pia mfuasi wa CCM jimbo la Kawe alivamiwa na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA.

Katika kata ya Makiba wakala wa CHADEMA, Rashid Jumanne na Mwenyekiti wake wa tawi la Valeska, ndugu Nickson Mbise walijeruhiwa vibaya kwa kushambuliwa na mapanga asubuhi wakielekea vituo vya kupigia kura.

Pia katibu wa ccm wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alilazwa hospitalini baadaya kushambuliwa na watuwanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA alipokuwa akiwapeleka mawakala wa chama hicho kwenye vituo vya kupigia kura.

Vitendo hivyo pia vimeripotiwa katika kata za Maswa, Nyabubinza na Simiyu

Mawakala katika vituo 8 kati ya vituo 13 walikamatwa na polisi ikiwemo diwani wa CHADEMA Zakayo Chacha Wangwe,
Kata ya Kimweri wilaya ya Meatu, ndugu diwani Emmanuel Mawadi akiwa na mawakala wawili wa chadema walivamiwa na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM na kukatwa mapanga.

Pia kiongozi wa CHADEMA katibu wa CHADEMA ubungo alikamatwa na polisi tangia tangia tarehe 25, pia mbunge Susan Kiwanga amekamatwa na polisi na yupo Morogoro na bado hajaachiwa.

Pia Meya wa Ubungo alikuwa ndiye wakala mkuu kata ya Saranga alikamatwa na polisi.

Pia mgombea wa Udiwani kata ya Sofi huko Malinyi alikamatwa na polisi alipotembelea kituo cha kupigia kura bila kutolewa sababu

Pia katika vituo 13 mawakala waliondolewa katika vituo vyao na kupelekwa katika vituo vya polisi.

Pia kata 6 za udiwani katika jimbo la Arumeru Mashariki, mawakala walitolewa nje wakati zoezi la upigaji kura likiendelea na kurudishwa baada ya masaa 4 na kufanya uchaguzi kuonekana usiwe huru na wa haki.

Pia mawakala wa CHADEMA walizuiliwa kuingia vituoni katika kata ya Saranga baada ya kunyimwa fomu za kuwatambulisha na mkurugenzi wa uchaguzi.

Kituo hicho kimetahadharisha matukio haya yasipokemewa yataathiri chaguzi zijazo kama uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kuwatisha wananchi wasishiriki.

No comments:

Post a Comment

Popular