Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema atawachukulia hatua wahandisi wazembe wa halmashauri wanaoshindwa kusimamia ipasavyo miradi ya barabara.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo wilayani Kiteto mkoani Manyara, akiwa ziarani kukagua miradi ya maendeleo.
Akizungumza leo Jumapili Novemba 5,2017 akikagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita 88.1 kutoka Kata ya Namelock hadi Kata ya Sunya, amesema hatawaonea huruma watendaji wazembe wa Serikali wasiotekeleza wajibu wao.
Amesema wahandisi wa halmashauri ndio wasimamizi wakuu wa miradi ya ujenzi, hivyo wanapaswa kuisimamia ipasavyo kwa kuwa Serikali inawekeza fedha nyingi.
"Kama mkandarasi anafanya uzembe kwenye mradi wa Serikali inapaswa afukuzwe kwa kuwa hizi Sh2 bilioni zinazotumika hapa zimetolewa na Serikali kwenye mradi huu utakaogharimu Sh6 bilioni," amesema
Waziri Jafo pia ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto lililopo mji mdogo wa Kibaya; kituo cha afya Engusero na Shule ya Sekondari Engusero.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la halmashauri amesema linatarajiwa kugharimu Sh4 bilioni hadi kukamilika.
Magessa amesema ujenzi unachelewa kwa sababu halmashauri imechelewea kupata fedha kutoka Serikali Kuu.
Amesema ujenzi ulianza Oktoba 26,2016 lakini ulisimama kwa muda wa miezi mitano kutokana na mkandarasi kukosa fedha.
Mbunge wa Kiteto, Emmanuel Papian amemshukuru waziri kwa kutembelea wilaya hiyo akisema amejionea changamoto zilizopo.

No comments:
Post a Comment