Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka na kusema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza mishahara ya wafanyakazi mwezi huu Novemba kama Rais Magufuli alivyoagiza
Dkt. Abbasi amesema hayo wakati akitoa tathmini ya miaka miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli toka alipoapishwa Novemba 5, 2015 na kusema kuanzia mwezi huu wafanyakazi wataongezewa mishahara yao.
"Mwezi huu mishahara ya wafanyakazi wa Serikali itaongezwa kama Rais Magufuli alivyoahidi" amesema Dkt. Hassan Abbasi.
Mbali na hilo Msemaji wa Serikali amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli wameweza kufanikisha kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina pia amedai ndani ya muda huo Serikali imeanzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa.

No comments:
Post a Comment