Serikali: Miaka miwili ya Rais Magufuli, tumeongeza ari na nidhamu kwa watumishi wa umma ,mapato yamepanda kutoka trion 9.9 mpaka 14 trion. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 5 November 2017

Serikali: Miaka miwili ya Rais Magufuli, tumeongeza ari na nidhamu kwa watumishi wa umma ,mapato yamepanda kutoka trion 9.9 mpaka 14 trion.

  "Katika miaka miwili hii tumefarijika kuona watanzania wengi wanaunga mkono mageuzi makubwa nchini"

    "Tunajivunia kuongezeka kwa ari na nidhamu kwa watumishi wa umma"

    "Mpaka sasa tumebaini watumishi hewa elfu ishirini ambao kama wangelipwa ingegharimu Tzs bil. 236"

    "Eneo lingine ni kubaini watumishi wenye vyeti feki 12,000 ambapo kama wangelipwa ingegharimu TZS Bil. 142.9"

    "Kwa mwezi Serikali inatumia Tzs Bil. 23 kwa mwezi kwa ajili ya Elimu Bure"

    "Serikali ilianzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa"

    "Miaka ya 2014-2015 safari za nje za watumishi na viongozi wa serikali ziligharimu sh. 216 bilioni"

    "Miaka miwili ya serikali ya awamu ya 5 safari za nje zimegharimu kiasi kisichozidi sh. 25 bilioni"

    "Makusanyo ya mwaka yameongezeka kutoka trilioni 9.9 mwaka 2015 hadi trilioni 14 mwaka 2017"

    "Uzalishaji wa madini ya Tanzanite na Almasi umeongezeka kutoka karati 15,000 - 18,000 hadi karati 28,000 - 32,000"

    "Kama nchi, safari ya kuelekea kujitegemea tumeshaianza kwa njia nyingi"

    "Kwa mwaka 2015, Bajeti ya dawa na vifaa tiba ilikua TZS Bil. 30, kwa miaka 2 bajeti imefikia TZS Bil. 261"

    "Katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli tumefanikiwa kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina"

    "Tupo kwenye awamu ya mageuzi, vyombo vya habari vinapaswa kuungana na matamanio ya wananchi"

    "Mkoani Arusha kuna mradi wa maji wa TZS Bil. 476 unaendelea na mingine ya TZS Tril.1.2 inaendelea katika miji 17"

    "Kuanzia mwisho wa mwezi huu watumishi wataanza kuongezewa mishahara na kupandisha madaraja, na kulipwa stahiki zao"

    "Katika sekta ya kilimo tumeondoa Tozo na Kodi nyingi zilizokuwa kero kwa watanzania"

    "Tumefanya udhibiti katika bei za mazao na juzi tumesikia Mtwara bei ya korosho imefika Tsh. 4100/= kwa kilo"

    "Wafanyakazi kwa sasa wanauhakika na misharaha ikifika tarehe 25 ya mwezi hela imeshaingia"

    "Kipande cha reli ya kisasa kinachojengwa kutoka Dar hadi Dom kitagharimu TZS Tril 7.1 ikiwa ni fedha za ndani"

    "Mradi wa Kinyerezi 2 wa megawati 240 uko katika 84% kukamilika, mtambo wa 1 wa megawati 30 utawashwa Desemba,2017"

    "Kuhusu ndege ni kama nilivyosema tunanunua ndege nne, kufika mwakani ndege zote tulizoagiza zitafika nchi"

    "Ndege Boing Dreamliner kuwasili July mwakani na zile za c-series kuwasili June mwakani"

    "Takwimu za mwaka 2017 za TIC na UNCTAD, katika nchi za EAC, Tanzania inaongoza kwa wawekezaji kutoka nje"
    

No comments:

Post a Comment

Popular