Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao.
Ametoa wito huo Juzi Oktoba 31, 2017 wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri utaifa wake.
"Tembea huku ukiringia nchi yako, wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, iseme vizuri kama ambavyo wengine wanasema vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo"alisema waziri mkuu Majaliwa.
Aliwataka wakumbuke kuweka akiba na wanapopata fursa watume fedha zao nyumbani ili zisaidie kuleta maendeleo.
"Ukipata kitu kidogo, rusha nyumbani, ukimpata mtu anayeweza kuleta tija, mlete nyumbani, nasi tutawapokea wewe na yeye", alisisitiza waziri mkuu Majaliwa.
"Tunawasisitiza muitangaze nchi yenu kwa mataifa mengine ili nao waone kuwa Tanzania ni mahala pa fursa, na akitaka kuwekeza ajue kuwa anawekeza mahala ambapo ni salama", alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

No comments:
Post a Comment