Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameitaka serikali kutoa taarifa kamili kuhusu kinachoendelea katika usaili pamoja utoaji wa mikopo kwa wananfunzi wa vyuo vikuu.
“Tunaomba kesho baada tu ya maswali serikali itoe tamko au taarifa kamili ya kuhusu nini kinachoendelea…,” alisema Spika Ndugai. Spika Ndugai ameyasema hayo wakati akitolea maelezo muongozo ulioombwa na Mbunge wa viti Maalum Martha Mlata (CCM) aliyeomba kuelezwa kwa nini baadhi ya wanafunzi walioomba kujiunga na vyuo vikuu pamoja na kuwa na sifa hawakupewa mkopo.
Spika Ndugai ameeleza kuwa suala hilo ni nyeti kabisa kwani wapo wanafunzi wengi ambao wanakumbwa na changamoto zikiwamo kulipia fedha ya usajili ili waweze kupata haki yao ya mkopo huku wengi wakiwa wanatokea katika familia zisizo na uwezo. “Jambo hili ni serious kabisa… wala siyo wa mwaka wa kwanza peke yake, na wengine pia.
Mwanafunzi akifika chuoni anatakiwa alipe kwanza fedha za kusajiliwa halafu ndiyo apate ile haki yake ya mkopo. Watoto hawa ni wa masikini…,” alisema. Mapema jana baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliokosa mikopo, walikusanyika katika ofisi za Bodi ya mikopo (HESLB) zilizopo Mwenge Jijini Dar es Salaam, wakishinikiza bodi hiyo iwape mikopo kwani wanazo sifa.
Meneja wa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo, Omega Ngole alipohojiwa alieleza kuwa bodi ya mikopo bado inalishuhulikia suala hilo na ifikapo ijumaa majibu yatakuwa yametolewa huku akieleza kuwa wamekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo wanafunzi wasio na sifa kuomba mikopo, na wengine kutothibitisha vyuo walivyochaguliwa.
Aidha Meneja Ngole aliwataka wanafunzi wote wenye sifa waliokosa mikopo watumie fursa iliyopo ya kukata rufaa ili waweze kushughulikiwa na kupata mikopo kama wanastahili.

No comments:
Post a Comment