Serikali imeweka utaratibu na bei mpya za upigaji picha katika daraja la nyerere kigamboni. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 9 November 2017

Serikali imeweka utaratibu na bei mpya za upigaji picha katika daraja la nyerere kigamboni.

 
 Baada ya kuwepo kwa mkanganyiko wa gharama za kupiga picha daraja la Nyerere Kigamboni, hatimaye Serikali imetangaza mchanganuo wa malipo ya huduma hiyo darajani hapo

Kaimu meneja mahusiano wa NSSF Salim Khalifan Kimaro, amesema Serikali imetoa utaratibu huo maalumu ambao watu wanaotaka huduma ya picha katika daraja hilo watautumia.

Uamuzi huo pia umezingatia suala zima la kulinda miundombinu ya daraja hilo pamoja na usalama wa raia wenyewe.

Utaratibu wa sasa wapiga picha wanalazimika kuomba kibali kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, kisha watapata maelekezo ya kufuata.

Aidha gharama za upigaji picha kwa matukio maalumu kama harusi, kutengeneza video za kwaya na wasanii wa muziki wa kawaida itakuwa ni Tsh 250,000 kwa saa moja na Tsh 125,000 kwa nusu saa.

Kwa upande wa wapiga picha za kawaida kwa mtu mmoja (selfie) hawatalipia gharama yeyote, lakini wametahadharishwa kuwa makini na usalama wao ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

No comments:

Post a Comment

Popular