Bashe: Nimepatwa hofu ya sisi viongozi badala ya kujadili hoja za msingi tunajadili ukanda. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 9 November 2017

Bashe: Nimepatwa hofu ya sisi viongozi badala ya kujadili hoja za msingi tunajadili ukanda.

 
 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameshangazwa na kitendo cha viongozi wenzake katika Bunge kushabikia mjadala unaohamasisha mgawanyiko wa Taifa kwa misingi ya Ukanda na Ukabila.

"Kwa mara ya kwanza nimepata hofu juu ya Taswira ya sisi viongozi. Badala ya kujadili mambo kwa Misingi ya Hoja Tumeanza kujadili Ukanda

"Bungeni leo (jana) nimeona Un holly discussion ambayo imejaa dhana ya kuligawa Taifa kwa misingi ya Ukanda na Ukabila

"Tangu, CCM toka 1957 mpaka Leo ilihimiza Umoja na Utaifa na kukemea uhalalishaji wowote wa kuligawa Taifa kwa Misingi ya Dini ukanda na tribe

"CCM, Chadema, CUF na NCCR tuliomo ndani ya Bunge hatuna haki yoyote ya kuanza kupandikiza mbegu ya kuligawa Taifa", Amesema Bashe.

No comments:

Post a Comment

Popular