Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya ziara katika bandari ya Dar es salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Mhe. John Pombe Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo ili kurahisisha utendaji kazi
Akiwa Bandarini IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi hilo Kikosi cha
Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo pamoja na kutenda haki ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja.
Hata hivyo IGP amewataka Polisi wasaidizi wanaofanya kazi bandarini hapo kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuendelea kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

No comments:
Post a Comment