Msafara wa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA - Bara Mhe. John J. Mnyika uliokuwa unatoka eneo la mkutano katika Kata ya Ndalambo, wilaya ya Momba mkoani Songwe umezuiwa na polisi na ghafla wakaanza kupiga mabomu ya machozi.
Huku wakivamia gari ya Mhe. Mnyika na kumchomoa dereva wake kisha walimpiga na kumpulizia usoni vitu visivyojulikana na baadaye Dereva Hugo alifanikiwa kuwakimbia Polisi japo mpaka sasa ametoweka haijulikani alipo na juhudi za kumtafuta zinafanyika.
Msafara huo ambao ulikuwa na Viongozi mbalimbali wa CHADEMA pamoja na Wabunge Mhe. Ernest Silinde (Mbunge wa Momba), Mhe. Frank Mwakajoka ( Mbunge wa Tunduma na Mhe. Risala Kabongo (Mbunge wa Vitu Maalumu Mkoa wa Songwe) ulizuiwa na Polisi ambao ghafla wakaanza kupiga mabomu ya machozi na pia licha ya kumpiga dereva wa Mnyika lakini pia wamechukua baadhi ya vitu katika gari hilo.

No comments:
Post a Comment