Magereza: Si kweli kwamba mfungwa akihukumiwa miaka 30 basi itahesabika usiku na mchana. - KULUNZI FIKRA

Thursday 2 November 2017

Magereza: Si kweli kwamba mfungwa akihukumiwa miaka 30 basi itahesabika usiku na mchana.

Studio za Radio Times Fm wapo SACP Charles Novat, ASP Deodatus Kazinja kutoka Jeshi la Magereza nchini wakieleza kuhusu hali Magereza na wafungwa.

Ufuatao ni mtiririko wa mahojiano yao na Waendeshaji wa kipindi cha Maisha Mseto.

Magereza hayapo ili kumuongezea mfungwa adhabu, tupo kuhakikisha mfungwa anatimiza adhabu aliyohukumiwa na mahakama. Ni jukumu letu kuhakikisha mfungwa anatoka na afya njema kama ambavyo aliingia nayo.

Wafungwa wote ni sawa, hakuna mfungwaa VIP. Huduma zote hupata sawa ispokuwa kwa wenye matatizo ya afya. Wafungwa wanapata taarifa, kuna TV na magazeti. Ni haki yao.

Nyampara ni kiongozi wa wafungwa ili kuongoza wafungwa wengine. Ni kiungo kati ya askari na mfungwa. Nyampara ni kama internal mechanism ya kuwafanya wafungwa wabadilike,

Nyampara hana mshahara isipokuwa anakuwa favoured kwenye vitu vidogo vidogo tu, ni sawa kama ilivyo kwa kiranja kwenye mashule.

Tunawatenga wafungwa kutegemea vitu mbalimbali ikiwemo umri wa mfungwa, jinsia na idadi ya vifungo.

Watu wanachanganya shule za maadilisho na magereza. Wanaopelekwa kule sio wafungwa. Mtoto haruhusiwi kupelekwa gerezani ispokuwa pale utata inapojitokeza.

Wafungwa/mahabusu wa kike wanapata huduma kama sheria inavyosema,Wapo watu binafsi wanaleta misaada kuwahudumia,hatukatai. Magereza hatuko kwa ajili ya kudhalilisha utu wa mfungwa.

Ufanisi wa mkuu wa gereza huonekana pale ambapo gereza linakabiliwa na changamoto. 1995 Wafungwa waliwahi kupiga kura, tulifanya utaratibu na wafungwa walipiga kura.

Changamoto ni kupata vituo vya jirani na gereza, pia wafungwa hujiandikisha kwenye vituo tofauti na magereza waliyopo. Sheria haikatazi mfungwa kupiga kura, ni utaratibu tu ambapo Tume ya Uchaguzi ikiandaa basi sisi tutafuata maelekezo.

Ikitokea mfungwa amefiwa na ndugu yake wa karibu, hakuna uwezekano wa kuhudhuria, utekelezaji wake ni mgumu kutokana na usalama

Sisi tuna vyuo vya ufundi, mfungwa anafundishwa ufundi stadi na kuzalisha vitu mbalimbali ikiwemo samani. Kutoa mitaji kwa wafungwa ni jambo jema lakini utekelezaji wake hautokuwa rahisi.

Kiutaratibu mfungwa akishiriki kwenye uzalishaji kuna kiwango flani kinatengwa kwa ajili yake ili kuwa motisha kwake.

Kuna wafungwa wana uwezo mbalimbali, inakuwa ngumu kutumia kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, mazingira na uhalisia. Gerezani ni sehemu ya mpito, tunategemea mfungwa arudi uraiani akiwa na mawazo ya kutokurudia makosa yake.

Kwa mazingira yetu mfungwa hawezi kukutana na mwenzi wake faragha, lazima iwepo miundombinu mahususi. Nchini kwetu haipo! Lakini tukiruhusu wakutane kimapenzi kati ya mfungwa wa kikee na mkmewe, vip akipata mimba? nani atalea?

Gerezani hakuna mazingira yanayoruhusu mapenzi ya jinsia moja, kama ikitokea wale ni binadamu, siwezi sema halitokei. Tumejitahidi kuweka mazingira ambayo hayatofanya hili jambo litokee, kama wakifanya ni haramu na makubaliano ya watu wawili.

Tuna utaratibu wa kuendeleza vipaji, ikitokea ana kipaji na gereza lina uwezo wa kukiendeleza basi tutamuingiza kwenye program. Kama kuna prodyuza anataka kurekodi nyimbo na wafungwa basi alete maombi na utaratibu utafuatwa.

Mfungwa akihukumiwa toka siku ya kwanza anapata 1/3 ya kifungo chake, lakini anapaswa aishi kwa nidhamu na kutii sheria. Si kweli kwamba mfungwa akihukumiwa miaka 30 basi itahesabika usiku na mchana.

Tunatoa wito kwa jamii kuwapa nafasi wafungwa wanaomaliza kifungo kuonyesha kwamba wamerekebishika kitabia, wasiwanyanyapae.

No comments:

Post a Comment

Popular