IGP Sirro atoa maagizo kuhusu watoto 1300 waliopotea. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 30 November 2017

IGP Sirro atoa maagizo kuhusu watoto 1300 waliopotea.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro amewataka wazazi kwa kushirikiana na walimu wilayani Kibiti na Rufiji, kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya kutoweka kwa wanafunzi zaidi ya 1,300 wakati wa matukio ya kiuhalifu yaliyotokea katika wilayani humo.

IGP Sirro amefanya ziara kikazi wilayani Kibaha, mkoani Pwani amezungumza na wazazi, walimu pamoja na viongozi wa mashirika ya umma, wazee maarufu, wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo.

Sirro amewataka wazazi kusaidiana na walimu wa shule za msingi na sekondari ambazo wanafunzi walikuwa ni watoro ama hawajaripoti shule kwa miezi kadhaa kutoa taarifa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.

Kamanda Sirro ameeleza kuwa taarifa ya wanafunzi zaidi ya 1,300 mkoani hapo kuwa ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.

No comments:

Post a Comment

Popular