Hatimaye Niki wa Pili apewa ushawishi wa kujiunga na chama cha siasa. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 22 November 2017

Hatimaye Niki wa Pili apewa ushawishi wa kujiunga na chama cha siasa.

 
Msanii NIki wa Pili ambey ni miongoni mwa wasanii wasomi nchini, ameitwa kujiunga na chama cha ACT Wazalendo, ili kuongeza nguvu na kukijenga zaidi chama hiko.

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Mhe  Zitto Zuberi Kabwe amemuandikia ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter kumuomba kufanya hivyo.
"Njoo ujenge Chama cha kijamaa bana acha mambo yako", ameandika Mhe Zitto Kabwe kwenye ukurasa wa Nikki wa pili.

Baada ya tweet ya Zitto Kabwe kumuomba Niki, Niki alimjibu kuwa chama cha kijamaa kinajengwa na watu wanyonge, bali yeye  kama mtu wa vyombo vya habari sio wa kuaminika kwani hawachelewi kuwauza.

"Chama cha kijamaa hujengwa na vugu vugu la wanyonge wenyewe, ni muwe tu na mkakati wa kuwaunganisha ki ideologia, umoja zao hizo za boda boda, machinga, wakulima, sisi watu wa media hatu kawii kuwauza sokoni kama nyanya", ameandika Niki wa Pili.

Mpaka sasa haijulikani msanii huyo ni mfuasi wa chama gani kutokana na kuonekana kuwa mwanaharakati wa masuala ya kisiasa na uchumi, na hajawahi kuonekana kwenye jukwaa la chama chochote kufanya kampeni.

No comments:

Post a Comment

Popular